Na Hussein Stambuli, Morogoro.

Waziri wa Nishati Mhe Dk Medard Kalemani ameagiza Ujenzi wa barabara ya ya lami ya kilometa 60 kutoka Fuga hadi eneo la mradi wa Julius Nyerere uanze sambamba na marekebisho ya barabara ya Ngerengere hadi Matambwe ili kurahisisha ufikishwaji wa mizigo kutoka Stesheni ya Fuga hadi kwenye mradi.

Waziri Kalemani amesema hayo baada ya kutembelea mradi huo mkubwa wa kuzalisha umeme kwa Julius Nyerere ikiwa ni awamu yake ya tisa kufanya hivyo, kwa lengo la kujionea maendeleo ya kazi zinazofanywa na Mkandarasi, kubaini changamoto za kiusimamizi na manufaa na fursa hasa kipindi cha utekelezaji Huku akiambatana na Mhandisi Brigedia Jenerali, Mahmoud Nssar, Naibu Waziri wa Ujenzi, Serikali ya Misri.
Jopo la wataalam wa masuala ya Nishati wakionngozana na Waziri wa Nishati Mhe Dk Medard Kalemani pamoja na mhandisi Brigedia Jenerali,Mahmoud Nssar, Naibu waziri wa ujenzi, Misri wakitembelea mradi wa umeme.
Waziri wa Nishati Mhe Dk Medard Kalemani katikati mhandisi Brigedia Jenerali,Mahmoud Nssar, naibu waziri wa ujenzi, Misri wakisikiliza maelezo kutoka kwa mratibu wa mradi,tanesco makao makuu stephen manda
Waziri wa Nishati Mhe Dk Medard Kalemani pamoja na mhandisi Brigedia Jenerali, Mahmoud Nssar, Naibu waziri wa ujenzi, Misri.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: