Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Songwe mkoani Mbeya kabla ya kuelekea mkoani Songwe kwa ajili ya ziara ya kikazi.

Rais Magufuli "Ampa tano" RC Chalamila kwa kuwacharaza viboko wanafunzi watukutu huko Mbeya.

Rais amemwagia sifa Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya kwa kuwaadhibu wanafunzi 14 wa shule ya sekondari Kiwanja iliyoko wilayani Chunya Mkoani Mbeya kwa kuwacharaza viboko vinne kila Mmoja kwa kumiliki simu za mkononi kinyume na Sheria na muongozo ya shule.

Sambamba na hilo Mkuu huyo wa Mkoa amewarudisha nyumbani wanafunzi wote 392 wa kidato cha tano na sita wa shule hiyo baada ya wenzao kuchoma Moto jengo la shule, ikielezwa kuwa tukio Hilo limetokea muda mfupi baaa ya wanafunzi hao 14 waliochapwa viboko kunywng'anwa simu hizo walizokuwa wanamiliki kinyume Cha Sheria. RC pia ameagiza wanafuzi hao watakaporejea shul eni Oktoba 28, 2019 wakiwa na sh. 200,000/- kila Mmoja huku wale 14 wakiakiwa kuja na sh.500,000/- kila Mmoja, vinginevyo watakamatwa na kufikishwa mahakamani kwa makosa wanayotuhumiwa nayo. Rais Magufuli ametoa pongezi hizo leo Oktoba 4, 2019 wakati akihutubia wananchi Mkoani Songwe
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: