Picha ikionyesha Mkuu Wilaya ya Arumeru Jerry Muro pamoja na kamati ya usalama ya Wilaya wakiendelea na kazi ya kumtafuta ,kijana mmoja alietambuliwa kwa jina la Samwel Gildati Mhina anaejishughulisha na kazi za kuongoza watalii anahofiwa kuzama katika ziwa momela.

Na Mwandishi Wetu.

UPEPO uliovuma ghafla katika Mkoa wa Arusha umesababisha kuzama kwa watu watatu wakiwemo watalii wawili huku mtu mmoja akihofiwa kupoteza maisha katika Ziwa Momela lililopo Hifadhi ya Taifa ya Arusha iliyopo wilayani Arumeru.

Kwa mujibu wa Mkuu Wilaya Arumeru Jerry Muro amesema kutokana na upepo huo mkali uliotokea jana saa nane mchana mtumbwi waliokuwa wanautumia watalii hao kutalii katika ziwa Momela ulipigwa na dhoruba ya upepo na kupinduka.

Amesema katika halmashauri ya Meru eneo la Momela watu watatu waliokolewa baada ya mitumbwi miwili waliokuwa wanautumia kupigwa na uppep mkali na kupinduka, ambapo kijana Samwel Mhina anaejishughulisha na kazi za kuongoza watalii anahofiwa kuzama katika ziwa hilo pamoja.Mtumbwi aliokuwa anaitumia haujapatikana mpaka.

Murro amesema Jeshi la Polisi pomoja na vikosi vya zimamoto na uokoaji kutoka mkoani na wilaya ya Arumeru vinaendelea na kazi ya kuwatafuta

"Mtakumbuka jana Oktoba 1, 2019 mchana Mkoa wetu wa Arusha ulikumbwa na dhoruba ya upepo mkali, ambao pamoja na maeneo mengine upepo huo ulienea mpaka katika maeneo ya Wilaya ya Arumeru.Umeleta madhara katika maeneo kadhaa,"amesema.

Amebainisha kuwa katika tukio hilo raia wawili wa nje waliokolewa mara baada ya mtumbwi wao kupigwa na dhoruba ya upepo na kupinduka waliokolewa wametambuliwa kwa majina ya Dk.Tuemper Bern John na Dk. Rosenberger ambao ni wa Ujerumani

Muro amesema kuwa katika kijiji cha Kimundo kata ya Nkoarisambu nyumba moja imeezuliwa paa , ambapo pia katika kijiji cha Ulong’aa kata ya Nkwandrua paa la choo cha shule ya msingi nalo liliezuliwa.

Amesema mpaka sasa baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki Dk. John Danielson pallangyo wako katika maeneo yaliyokumbwa na changamoto
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: