Kaimu Mkurugenzi wa PCI, Jennifer Waugaman akiwa na Mratibu wa PCI ncuini, John Lafa(kulia) wakipewa zawadi baada ya kuzindua mradi huo.
Mwandishi wetu, Monduli.

Wafugaji wa wilayani tatu za mkoa wa Arusha,watakuwa wakifikia malisho na maji ya mifugo yao kwa kutuma ujumbe wa simu kuulizia eneo lenye maji na malisho na kujulishwa.

Mradi huu umezinduliwa jana na shirika la kimataifa la PCI ,l, katika kijiji cha Arkaria wilayani Monduli na utatekelezwa pia wilaya za Longido na Ngorongoro ambazo zina idadi kubwa ya mifugo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Rais wa PCI, Carrie Hetessler-Radelet alisema, wafugaji kupitia simu zao za mkononi, baada yakupakuwa application ya Afriscout watatuma bure ujumbe kwenda15054 kuuliza malisho na maji.

Hetessler –Radalet amesema baada ya kuuliza,mtandao huo utaonesha ramani za sehemu ya maji na malisho ambayo imepigwa angani.

Amesema mradi huo, utawezesha wafugaji kuacha kusafiri muda mrefu kusaka malisho, kuharibu mazingira lakini pia utapunguza vifo vya mifugo na adha ya wafugaji kushindwa kufanya shughuli nyingine za kiuchumi.

Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo, Jennifer Waungaman amesema mradi huo ambao unatarajiwa kuwanufaisha sana wafugaji.

“Tunawaomba wafugaji kutumia huduma hii ambayo pia itawasaidia kusimamia vizuri nyanda za malisho yao” alisema.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Kaimu mkurugenzi endeshji wa malisho na vyakula vya mifugo,Dk Asimwe Rwiguza alisema mradi ho una manufaa makubwa kwa wafugaji na amelitaka shirika hilo kupanua huduma hiyo nchi nzima.

Mfugaji John Laizer amesema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwao na itaondoa tatizo la mifugo kufariki wakati wa kiangazi na migogoro na wakulima.

Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Monduli, Joseph Rutabingwa alisema halmashauri ya Monduli itaupa ushirikiano mradi huo ili wafugaji wanufaike zaidi.

Mradi huu pia unatekelezwa katika nchi tatu barani ambazo ni Tanzania, Kenya na Ethiopia na shirika hilo linafanya kazi katika nchi 16 Duniani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: