Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Nzega vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Budushi, Nzega Vijijini mara baada ya kufika shuleni hapo akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kuhamasisha maendeleo, kuzungumza na wananchi na kutatua kero zao katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Nzega Vijijini.
 Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Nzega vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Budushi katika jimbo la Nzega Vijijini alipofanya mkutano wa kuimarisha Chama na kutatua kero za wananchi.

Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Nzega vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa na viongozi wengine wa CCM kutoka katika Kata mbalimbali za jimbo la Nzega Vijijini wakitazama Kadi za wanachama 100 wa CHADEMA waliohamia CCM kufuatia kuridhishwa na Utendaji Kazi wa Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika Kata ya Ndala, Nzega Vijijini.

Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Nzega vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimpokea na kumkaribisha katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Lucas Kitambi Maselele, Mwenyekiti Mstaafu na Katibu wa CHADEMA jimbo la Nzega vijijini mara baada ya kujiunga rasmi na CCM. PICHA – Aron Msigwa – Nzega.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: