Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimetoa mafunzo ya Siku tano kwa wafanyakazi wanataaluma wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) Mkoani Iringa, jinsi ya Kupata Makala kutoka katika Tasnifu zao. (On How to turn a Thesis/Dissertation into a Journal Article). Mafunzo hayo yalianza rasmi tarehe 2 Novemba 2019 na yanatarajiwa kumalizika tarehe 5 Novemba, 2019.
 Mkurugezi wa Kurugenzi ya Huduma kwa Umma Dkt. Mona Mwakalinga, pamoja na Dr. Fikira Kimbokota wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa wakifuatilia jambo wakati wa mafunzo hayo chuoni hapo.
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. A Makuliko na Prof. A Mtembei wa Chuo Kikuu Dar es Salaam wakiteta jambo wakati wa Mafunzo yanayoendelea katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa.( MUCE)
 Mmoja wa wanataaluma wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, akiuliza jambo wakati wa mafunzo Kupata Makala kutoka katika Tasnifu zao. (How to turn a Thesis / Dissertation into a Journal Article).
Baadhi ya wanataaluma wakifuatilia kwa makini mafunzo ya Kupata Makala kutoka katika Tasnifu zao yaani (How to turn a Thesis / Dissertation into a Journal Article). Yaliyoandaliwa na Kurugenzi ya Huduma kwa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: