Na Emmanuel J. Shilatu

Napenda kuungana na Mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutimiza miaka 4 tangu achaguliwe kuwa Rais.

Naam! Ni miaka 4 ya Rais Magufuli Ikulu ambapo sote mashuhuda wa haya:-

1. Ameisimamia na kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuhakikisha amani na usalama wa nchi unazidi kuimarika. Amekomesha kabisa matukio aliyokutana nayo awali anaingia madarakani ya ujambazi, migomo na mauaji ndani ya jamii. Hata Umoja wa Mataifa (UN) ulishampongeza Rais Dkt. Magufuli kwa kudumisha amani na usalama ndani na nje ya Tanzania.

2. Amekuwa Mlezi na msaada kwa Watoto wa Watanzania wanyonge ambapo Serikali yake imewawezesha kusoma elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne. Zaidi ya Tsh. Bilioni 937 zimetumika tangu mwaka 2016.

3. Ameonyesha kivitendo kuchukia na kukemea rushwa na ufisadi nchini. Ambapo leo nchi ya Tanzania inashika nafasi ya pili (2) kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

4. Ametekeleza kivitendo ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ya kuhamia Dodoma. Leo hii Serikali nzima mpaka yeye Rais Magufuli amehamia Dodoma, makao makuu ya nchi.

5. Ameongeza na kusimamia mapato ya nchi kutoka wastanj wa makusanyo ya Tsh. Bilioni 800 hadi kufikia wastani wa makusanyo ya Tsh. Trilioni 1.7

6. Rais Magufuli amejipambanua kivitendo juu ya sera ya Tanzania ya viwanda ambapo ndani ya miaka 4 zaidi ya viwanda vikubwa na vidogo 4000 vimejengwa.

7. Uwajibikaji na uadilifu kwa Watumishi wa umma umeongezeka na kuimarika sana. Hakuna majivuno, uchelewaji makazini, ugoigoi badala yake huduma kwenye ofisi za umma zimeimarika sana.

8. Rais Magufuli amesimama kidete kufufua mashirika yetu ya umma ambayo yalikuwa hoi bin taabani. Leo hii shirika la simu Tanzania limefufuka; Shirika la ndege nchini ATCL nalo pia limefufuka kwa kununuliwa ndege mpya 7 za kisasa na nyingine 4 zimeagizwa. Nani kama Rais Magufuli?

9. Serikali imeanzisha na kufanya miradi mikubwa ya kimkakati nchini. Mathalani ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme kwa kiwango cha standard gauge unaogharimu zaidi ya Trilioni 7.1; Mradi wa ujenzi wa umeme wa Mto Rufiji utakaozalisha Megawatts 2115; Ujenzi wa flyovers Tazara, Ubungo na sealander.

10. Kwa mara ya kwanza tangu Dunia iumbwe tumeshuhudia uwazi kwenye mikataba ya madini na maboresho ya Sheria za madini kulinufaisha Taifa. Hii imeleta matokeo chanya ya ongezeko la makusanyo yatokanayo na madini kupitia mfumo mpya wa uuzaji na ununuzi kwenye masoko ya madini. Leo hii wawekezaji wa madini wanabanwa na tija ya mapato imeongezeka.

11. Ukuaji wa uchumi umezidi kuongezeka kwa kasi kutoka asilimia 5.7 kwa mwaka 2015 hadi kufikia ukuaji wa asilimia 7.2 mpaka sasa. Ukuaji huu unaifanya Tanzania kuwa nchi ya pili Barani Afrika kwa kasi ya ukuaji kiuchumi.

12. Ujenzi wa hospitali 73 za wilaya na vituo vya afya zaidi ya 352 nchini vinavyotoa huduma ya upasuaji. Ujenzi huo umeenda sanjali na uimarushwaji wa vifaa tiba vya kisasa na Madaktari wa kutosha. Leo hii upasuaji mkubwa na tiba kubwa ambazo awali ilikuwa zinapatikana nje ya nchi sasa zinafanyika nchini.

Hakika ni miaka 4 ya uchapakazi, uzalendo, ufuatiliaji na uadilifu katika ujenzi na uletaji matokeo chanya kwa Taifa. Watanzania tumekuelewa, tunakushukuru na tupo pamoja kwani Tanzania moya tunaiona na tunaiishi ndani ya miaka 4 ya uongozi wako.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais Magufuli kwa kumpatia ulinzi, afya njema na maarifa zaidi.

Shilatu E.J
0767488622
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: