Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi wa Msamvu mkoani Morogoro mara baada ya kusimama.
Sehemu ya Wananchi wa Msamvu mkoani Morogoro waliokuwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara aliposimama katika eneo hilo. PICHA NA IKULU.

Rais Dkt John Pombe Magufuli amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Anold Kihaule kwenda mkoani Morogoro leo na ikiwezekana akae Mkoani humo hata siku tatu ili kushughulikia tatizo la wananchi wengi kukosa vitambulisho vya Taifa huku Mkoa mzima ukiwa na Ofisi moja pekee ya NIDA.

“Nimemtaka Mkurugenzi Mkuu NIDA afike hapa Morogoro ashughulikie hii changamoto ya vitambulisho na nataka huduma hii iende kila Wilaya, haiwezekani watu wasafiri kutoka Wilayani kuja mjini au muwape nauli na hela ya Gesti,na hili litazamwe Nchi nzima Watu wapewe vitambulisho”, amesema Rais Magufuli.

Amesema watu wanataka kusajili laini zao za simu na mambo mengine lakini zoezi la vitambulisho linacheleweshwa na watu wachache, suala la NIDA linaenda polepole sana, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA nitahitaji unipe na tathmini ya zoezi lote Nchi nzima ", amesema Rais Magufuli.

Aidha, amesema serikali yake haitawapangia bei ya kuuzia mahindi yao wakulima, kwani gharama za Kilimo haikuwasaidia. Amesema hayo leo hii akiwa Msamvu mjini humo aliposimama kusalimia wananchi akiwa njiani kwenda jijini Dodoma.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: