Mkuu wa kitengo cha Huduma za Ufundi na Kinga ya Mionzi, Dennis Mwalongo akizungumza na wafanyabiashara wa zao la kahawa kwenye mnada uliofanyika leo tarehe 21 wilaya ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro kuhusiana na upimaji wa mionzi kwenye Kahawa kwa lengo la kuhakikisha Tanzania inabakia kwenye soko la kahawa ikiwa na ubora na isiyo na vimelea vya uchafuzi wa mionzi
Wafanyabiashara wa zao la kahawa wakimsikiliza kwa makini mkuu wa kitengo cha huduma za ufundi na kinga ya mionzi wa TAEC alipokuwa akizungumza nao kwenye mnada uliofanyika wilaya ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro.

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imetoa elimu juu ya umuhimu wa upimaji wa mionzi katika zao la kahawa kwa wafanyabiashara wa zao hilo kwenye soko la mnada uliofanyika wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro leo tarehe 21/11/2019.

Mnada huo umewashirikisha wafanyabiashara mbali mbali wanaosafirisha kahawa ndani na nje ya nchi ambapo wameweza kupata uelewa wa sababu za upimaji wa mionzi kwenye kahawa na utaratibu mzima wa upatikanaji wa vibali vya kusafirisha zao hilo nje ya nchi bila kutumia mawakala.

Mkuu wa kitengo cha Huduma za Ufundi na Kinga ya Mionzi, Dennis Mwalongo amewaambia wafanyabiashara hao kuwa lengo la kuhakikisha Tanzania inaendelea kubakia katika soko la kahawa yenye ubora na isiyo na vimelea vya uchafuzi wa mionzi.

“Tunawaelewesha hapa sababu za kupima mionzi kwenye kahawa kwani ni muhimu sisi kama Taasisi tuna wajibu wa kuhakikisha madhara yatokanayo na mionzi hayatokei ”alisema Mwalongo.

Sheria Na. 7 ya mwaka 2003 ya Nguvu za Atomiki Tanzania imeipa mamlaka TAEC kudhibiti matumizi salama ya mionzi hapa nchini.

TAEC itaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara mbali mbali nchini juu ya kazi zake kwa lengo la kusaidia kutoa uelewa zaidi juu ya upimaji wa mionzi kwenye bidhaa mbali mbali zinazosafirishwa ndani na nje ya nchi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: