Mkuu wa idara ya mikakati, Squad Digital Parusha Partab,  akisikiliza katika Mkutano wa Reboot Tanzania iliyoandaliwa na WPP Scangroup jijini Dar es Salaam.
Stanley Kafu, Meneja Masoko wa Exim Bank akisikiliza katika Mkutano wa Reboot Tanzania iliyoandaliwa na WPP Scangroup jijini Dar es Salaam.
Benji Fernandez, Mkurugenzi Mkuu wa Nala, Bw. David Minja, Mkurugenzi Mkuu wa Unilever na Bw. Francis Majige Nanai, Mkurugenzi Mkuu wa Mwananchi Communications katika mkutano wa Reboot Tanzania iliyoandaliwa na WPP Scangroup jijini Dar es Salaam.
Idriss Sultan, Omary Tambwe ( Lil Ommy) na Webiro Wassira (Wakazi) katika mkutano wa Reboot Tanzaniailiyoandaliwa na WPP Scangroup jijini Dar es Salaam.

WPP Scangroup leo imezindua mkutano ya kwanza kuhusiana na mabadiliko ya kidigitali. 

WPP Scangroup ilikuwa na mipango ya kuendeleza mazugumzo ya kuchochea mabadiliko ya kibiashara katika ulimwengu wa kidigitali. 

Mkutano huu ni wa kwanza kufanyika nchini Tanzania, ya kwanza ilifanyika nchini Kenya mwaka 2018 na ilikusanya makampuni makubwa katika ulimwengu wakibiashara nchini Kenya.

Tuitazama mazingira ya kibiashara tunaona kwamba kumekuwa na mabadiliko yakiongezewa na watu wanaotumia mtandao na mawasiliano. Mawazo ya watazamaji wetu yanabadilika na namna za zamani ambazo tulikuwa tunatumia kupeleka taarifa zimebadilika.

Kama kampuni ya WPP Scangroup, mkakati wetu ni kuwa kiongozi katika eneo la teknolojia na ubunifu. Tunataka kuingiza toleo rahisi, bora lililobuniwa ili kukamata fursa za soko zinazobadilika, na muundo ulioratibiwa uliojengwa na mahitaji ya wateja wetu.

Mkutano huu ambao uliwakutanisha Mkurugenzi Mkuu wa Standard Chartered Bank, Bw. Aljamair Riaz, Bw. Benji Fernandez, Mkurugenzi Mkuu wa Nala, Bw. David Minja, Mkurugenzi Mkuu wa Unilever na Bw. Francis Majige Nanai, Mkurugenzi Mkuu wa Mwananchi Communications. 

Katika mazugumzo yao Bw. Aljamair Riaz alisema kutokana na mabadiriko ya hali ya kidigitali benki ya Standard Chartered Bank wamebadilisha mkakati yao na kufuata upepo wa kidigitali. 

Aliendelea kusema ‘Hapo mwanzo gharama ya ununuzi ilikuwa juu. Lakini tulivyobadilisha na kwenda kidigitali, tumeweza kuokoa pesa na kuwaongezea wateja katika bidhaa mbali mbali. 

Aliongeza kuwa kwasasa mabadiriko ya kidigitali yamesababisha nchini Hong Kong kuzinduliwa kwa benki ya kidigitali tu iitwayo ‘Virtual bank’.

Kampuni ya WPP Scangroup pia iliwaalika influencers ambao ni mashuhuri ambao wako katikati mabadiliko ya kidigitali. Bw Webiro Wassira ambaye anajulikana kama Wakazi alisema ‘ kama influencer mtu anatakiwa kuuza mtindo ya maisha yake na kuwa mtindo huo wa maisha. Ni utamaduni.’ Omary Tambwe ambaye anajulikana kama Lil Ommy, yeye ni mtangazaji wa Times FM na hivi karibuni alishinda tuzo na mtangazaji bora na mkaribishaji bora alisema kuna utofauti ya kuwa na followers wengi na ujijengea brand.

Manish Sardana, Mkurugenzi Mkuu wa Squad Digital, alisema Kuja kwa umri wa dijitali kumetufanya sisi kama Biashara kufikiria mikakati yetu linapokuja suala la matangazo. 

Watazamaji wetu walengwa wanafikiria tofauti kwa sababu ya hali hii ya media za kijamii
Hapa ndipo tunapoingia na kuamini kuwa ni muhimu kuwajulisha na kuelimisha washirika wetu wa biashara njia hii kupitia wakati huu wa ajabu.

Mkutano huu ulikuwa na wasemaji kutoka makampuni mbali mbali za ki digitali kama Google, Squad Digital and Group M. WPP, Scangroup itapenda kuwa na mkutano kama huu kila mwaka .
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: