Mhifadhi kitengo cha ujirani mwema Zabron Mtwelve akizungumza na waandishi wa habari wa mikoa ya nyanda za juu kusini waliofanya ziara ya katika hifadhi ya taifa ya Serengeti kwa lengo la kujifunza maswala ya utalii.
NA FREDY MGUNDA, SERENGETI.

Hali ya umasikini ya wananchi wa wanaoizunguka hifadhi ya taifa ya Serengeti ndio ilikuwa chanzo cha wananchi kujihusisha na ujangili wa wanyama pori waliopo katika hifadhi hiyo kwa kiasi kikuwa kwa kuwa walikuwa hawana shughuli za kuwaingizia kipato.

Akizungumza na waandishi wa habari wa mikoa ya nyanda za juu kusini waliofanya ziara ya katika hifadhi ya taifa ya Serengeti kwa lengo la kujifunza maswala ya utalii,mhifadhi kitengo cha ujirani mwema Zabron Mtwelve alisema kuwa baada ya kufanya utafiti na kugundua kuwa umaskini wa mtu moja moja ni chanzo cha vitendo vya ujangili na waliamua kuanzisha Benki ya COCOBA.

“Baada ya kubaini umaskini wa kipato kwa wananchi wanaozunguka hifadhi ya Serengeti tulianzisha miradi ya mbalimbali ya kiuchumi kwa lengo la kuwaokoa kiuchumi wananchi hivyo moja ya mradi tulioanzisha ni mradi wa Benkiya hifadhi ya jamii (COCOBA) ili wananchi waondokane na vitendo vya ujangili katika hifadhi hiyo” alisema.

Mtwelve alisema mara baada ya kutoa elimu ya Benki hiyo na kutoa elimu ya madhara ya ujangili katika hifadhi ya Serengeti vitendo vya ujangili vimepungua kwa kiasi kikubwa kiasi kwamba ongezeko la mnyama Tembo limekuwa kubwa hivyo kuashiria kuwa ujangili umepungua.

“Tuligundua kuwa umasikini mtu moja moja ni tatizo linalochangia wananchi wengi kuingia kwenye hifadhi ya Serengeti na kufanya vitendo vya ujangili hivyo shirika kwa kutumia kitengo cha ujirani mwema tulianzisha miradi na mmoja ya mradi huo ni huu wa COCOBA ambao unasaidia wananchi kuinua uchumi na kuacha kutegemea ujangili katika hifadhi hiyo” alisema Mtwelve

Mtwelve Mbali na mradi huo wa Benki ya jamii bali kuna miradi kama ya ufugaji nyuki ambayo wamekuwa wakiitekeleza katika wilaya za Bariadi,Bunda na Tarime kwa lengo la kuendelea kuinua uchumi kwa wananchi na kupunguza vitendo vya ujangili kwa wanyama ambao wapo katika hifadhi hiyo.

“Kwa sasa hifadhi ya taifa ya Serengeti mkoani mara imefanikiwa kupunguza vitendo vya ujangili mara baada ya kuanzisha kitengo cha ujiarani mwema kwa vijiji vyote vinavyoizunguka hifadhi hiyo ya Serengeti” alisema Mtwelve

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Rebecca Msambusi alisema kuwa vitendo vya ujangili vimepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na elimu ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara kwa wananchi wote ili kuendelea kuitunza na kuilinda hifadhi hiyo.

“Tumekuwa tukitoa elimu mara kwa mara juu ya madhara ya vitendo vya ujangili vinavyoathiri uchumi wan chi na kwa mwananchi moja moja na tumewaeleza faida ya uhifadhi wa wanyama pori wetu ndio maana vitendo vya ujangili vimepungua” alisema Msambusi

Msambusi aliongeza kuwa hali ya utalii katika wilaya ya Serengeti imekuwa na watalii wanazidi kuongezeka kila uchwao na uchumi unakuwa kutokana na wananchi kuwa na elimu ya uhifadhi ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: