Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA AFRICA) na Spika wa Bunge la Kenya, Justin Muturi akiongoza kikao Chama hicho kilichofanyika mapema leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai (wa kwanza kushoto) pamoja na Wajumbe kutoka Nigeria, Kenya, Uganda na Namibia.
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai (wa kwanza kushoto) akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA AFRICA). Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA AFRICA) na Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi na kushoto ni Wajumbe wa Kamati hiyo.
Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akifurahia jambo na Spika wa Bunge la Kenya Mhe. Justin Muturi (kulia) wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA AFRICA) Jijini Dar es Salaam
Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto) akisalimiana na Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA AFRICA) ambao pia ni Wabunge kutoka Namibia, Nigeria na Uganda. PICHA NA BUNGE.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: