RAIS wa Jamhuri ya Muungano w Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amerejesha wanyamapori katika bustani za Ikulu Jijini Dar es Salaam hali iliyofanya madhari ya Ikulu kupendeza na kuvutia.
Wanyama waliopo katika bustani hizo ni pamoja na Pundamilia, Pofu, Swala, Digidigi, Tausi, Mbuni, Tumbili, Kanga, Batamaji na wengine.
Awali wanyamapori hao walifugwa kwa idadi kubwa wakati wa Uongozi wa Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na baadaye walitoweka hadi mwaka 2017 walipoanza kurejeshwa na Mhe. Rais Magufuli.
Mbuni
Pundamilia.
Tausi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: