Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) nchini Tanzania limesema litafunga bwawa la majitaka vingunguti kwa muda wa siku 30 kuanzia Jumatatu Machi 23, 2020 hadi Aprili 24, 2020.


Taarifa ya Ofisi ya Mawasiliano ya Dawasa iliyotolewa leo Ijumaa Machi 20, 2020 imesema sababu za kufunga bwawa hilo ni kuruhusu ukarabati wa bwawa la kwanza eneo la kupokea majitaka kwa magari.

Dawasa imewataka waendesha magari ya kunyonya majitaka, huduma ya umwagaji majitaka itaendelea katika mabwawa ya Kurasini maarufu kama Shimo la Udongo yaliyopo Wilaya ya Temeke jijini humo.

“Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza,” imeeleza taarifa hiyo
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: