Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi ndugu Christopher D. Kadio (wa nne toka kushoto ) akimkaribisha Mkuu wa Msafara wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,ambaye ni Mbunge wa Zanzibar Jimbo la Uzini ndugu Salum Rehani(wa nne toka kulia) walipowasili eneo la Mradi, Msalato. Wa tatu toka kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza Selemani Mzee.

Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi ndugu Christopher D. Kadio akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Msafara kuzungumza na viongozi wa Jeshi la Magereza pamoja na wajenzi wa mradi

Mkadiriaji Mkuu wa Ujenzi Makao Makuu ya Magereza Kamishna Msaidizi Aaron Lunyungu akitoa maelezo ya ramani ya mradi kwa Mkuu wa Msafara wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,ambaye ni Mbunge wa Zanzibar Jimbo la Uzini ndugu Salum Rehani.

Msimamizi Mkuu wa Mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha Useremala Gereza Msalato Mrakibu Bonanza Malata akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.Picha zote na Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Dodoma.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: