Mwimbaji wa Muziki wa Dansi Mwinjuma Muumini (Kocha) akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam wakati akitambulisha bendi yake mpya iitwayo Sadai sambamba na wanamuziki wa bendi hiyo.
 Rapa wa muziki wa Dansi Fugerson akizungumza machache wakati wa utambulisho.
Mwimbaji wa muziki wa dansi Mubela akitoa kionjo.
Mwimbaji wa muziki wa dansi Rama Pentagon akitoa kionjo.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mwimbaji wa Muziki wa Dansi Mwinjuma Muumini (Kocha) ametambulisha bendi yake mpya iitwayo Shadai wana Tikisa Tikisa yenye makazi yake Bagamoyo, Pwani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwanamuziki Mwinjima amesema kuwa bendi yao ni mpya na imeweza kusajili wanamuziki tofauti toka bendi mbali mbali.

'Nimekaa nikajipanga nimekuja upya na bendi yangu baada ya ukimya wa muda mrefu mno hivyo naomba Watanzania mnipokee kwa mikono miwili,' amesema Mwimbaji Muumini Mwinjuma.

Aliongeza kuwa kwa kipindi chote ambacho amekuwa akijinoa na bendi yake mpya ya Shadai na kuingia studio kufanikiwa kurekodi albamu aliyoipatia jina la 'Nimefulia'.

Ujio wangu huu wa Nimefulia umeweza kunishusha cheo changu na wale wote waliozoea kunitambua Muumini Mwinjuma a.k.a Kocha Wa Dunia nimeliondoa na kwa sasa niite Kocha tu.

Amesema kuwa bendi ya Sadai inatarajiwa kuzinduliwa jijini Dodoma mwishoni mwa mwezi huu katika Ukumbi wa 4G ambapo bendi ya Gold, bendi ya Sky na Bendi na Badi Bakule, mpaka sasa wameshaandaa Albabu ya Nimefulia iliyobeba nyimbo 8, ikiwemo Nimefulia, Nitumbue, Alikasusu, Mwanadamu Halidhiki.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: