WAUMINI wa Dini ya Kiislam wakiwa katika Ibada ya kuusalia Mwili wa Marehemu Marin Hassan Marin, Mwandishi wa Habari Muandamiziu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) sala na dua hiyo imefanyika katiuka Msikiti wa KMKM Kibweni Wilaya ya Magharibi”A” Unguja leo 2/4./2020,saa nne na kuzikwa katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar. (Picha na Othman Maulid).
MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Ayoub Rioba akizungumza na kutoa shukrani baada ya maziko ya mfanyakazi wake Mwadishi Muandamizi Marehemu Marin Hassan Marin, yaliofanyika katika makaburi ya mwanakwerekwe Jijini Zanzibar. (Picha na Othman Maulid).
AZIRI wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabot Kombo akizungumza na kutoa shukrani kwa niaba ya Wizara yake wakati wa hafla ya maziko ya Mwandishi wa Habari Muandamizi Tanzania Marehemu Marin Hassan Marin, yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar. (Picha na Othman Maulid).
MWAKILISHI wa Familia ya Marehemu akitoa neno la shukrani kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano wao katika kufanika msiba huo. (Picha na Othman Maulid).
WANANCHI wakibeba Jeneza lililokuwa na Mwili wa Marehemu Marin Hassan Marin, wakitoka nyumbani kwa marehemu na kuelekea katika Msikiti wa Kibweni KMKM kwa ajili ya kuombea dua kwa ajili ya maziko yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar. (Picha na Othman Maulid).
MAWAZIRI wa Habari wa SMT na SMZ. Kushoto Waziri Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, wakiwasili katika viwanja vya Msikiti wa Kibweni KMKM kuhudhuria maziko ya Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Marin Hassan Marin, yaliofanyika leo 2/4/2020 na kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi “B” Unguja. (Picha na Othman Maulid).
WANAICHI na Waumini wa Kiislam wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa maziko ya Marehemu Marin Hassan Marin Mwandishi wa Habari Muandamizi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) yaliofanytika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 2/4/2020. (Picha na Othman Maulid)
WAUMINI na Wananchi wakishiriki katika kisomo cha Hitma na Dua kumuombea Marehemu Marin Hassan Marin, iliofanyika nyumbani kwao Kibweni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja wakati wa hafla hiyo ya maziko yaliofanyika leo 2/4/2020 saa nne asubuhi na kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar. (Picha na Othman Maulid).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: