Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano Isack Kamwelwe amezindua majaribio ya  awali ya mfumo wa ukataji tiketi za mabasi kwa
njia ya mtandao nchini utakao simamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Aridhini (LATRA)
 
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano Isack Kamwelwe
Waziri Kamwelwe amezindua
mfumo huo jijini Dar Es salaam ambapo amesema kuwa mfumo huo uliotengenezwa na
Kituo cha Taifa cha Kutunza Taarifa (NIDC) utasaidia kupunguza msongamano
katika vituo na kurahisisha huduma ya ukataji tiketi kwa wasafiri.

“Mfumo huu wa tiketi mtandao
utatatua changamaoto za muda mrefu katika sekta ya usafiri,  kwani utakuwa na taarifa zote muhimu ambazo
zinaweza kutumiwa na taasisi kama Jeshi la Polisi, Uhamiaji na Mamlaka ya
mapato Tanzania(TRA) ambazo zinahusika na takwimu, sera na utafiti” Amesema
Waziri Kamwelwe
Mkurugenzi
Mkuu wa LATRA Gilliard Ngewe
Waziri Kamwelwe amesema kuwa
mfumo huo unafaida kwa wamiliki wa mabasi na watumiaji wa usafiri, ambapo utaondoa
upotevu wa mapato kwa wamiliki yaliyokuwa yanapotea kwenye mikono ya wapiga
debe.

Waziri amesema mfumo huo upo
tayari kutumika kwa majaribio hadi mwisho wa mwezi juni 2020 kwa usafiri wa
mabasi ya masafa marefu na ifikapo septemba 2020 utekelezaji wa mfumo huo utaanza
kwenye mabasi ya mjini.

Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkuu wa LATRA Gilliard Ngewe, amesema kuwa matumizi ya tiketi mtandao yataleta
mabadiliko makubwa katika sekta ya usafirishaji nchini kwani watoa
huduma na mawakala hawataweza kuwadanganya wamiliki wa mabasi kwani taarifa
zitakuwepo kwenye mfumo.“Suala la kumfungia tajiri hesabu
halitakuwepo kwani tajiri atajifungia hesabu yeye mwenyewe”Amesema Ngewe

Amesma kuwa matumizi ya tiketi  mtandao yataondoa orodha ya abiria iliyokuwa inapigwa muhuri na Jeshi la
Polisi kwani orodha hiyo itapatikana kwa njia ya mtandao.

Ameongeza kuwa  suala la abiria kulanguliwa nauli kila ifikapo
kipindi cha mwisho wa mwaka limekwihsa kwani abiria anaweza kukata tiketi kwa kutumia simu yake ya mkoni bila kufika
kituo cha mabasi.

 Ngewe amesema kuwa LATRA imejipanga kusimamia mfumo huo kikamilifu kwani kutakuwa na kituo maalum cha kutoa huduma kwa wateja ambapo wataweza kupiga simu na kupatiwa huduma kwa saa 24 kwa kupiga namba  0800110150.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: