Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania George Mathen

Kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania leo imetangaza kupunguza gharama za huduma mawasiliano ya intaneti ili kuwapa wateja wake uhuru zaidi wa kutumia mtandao wa intaneti wenye kasi wa Airtel 4G popote walipo.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam ilisema kuwa kuanzia leo, Airtel Tanzania imepunguza zaidi gharama ya huduma za intaneti ili kuwanufaisha wateja, Gharama hizo zimepunguzwa kwa asilimia 80 na kufikia shilingi 5 tu kwa kila MB moja. Kabla ya hapo, MB moja ya intaneti ilikuwa ikitozwa shilingi 40. Wateja wa Airtel kuanzia sasa wanaweza kufurahia unafuu huu katika orodha ya huduma yaani menu ya Smartphone zao.

Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania George Mathen amenukuliwa akisema, “Matumizi ya intaneti kwa wateja wetu yameongezeka sana na tunayo furaha kuwatangazia rasmi wateja wetu na wale wanaotaka kujiunga na Airtel ili waje kufaidika na gharama hizi nafuu sasa. Ni Imani yetu kuwa gharama hizi nafuu zaidi za shilingi 5 kwali MB moja zitawapa uhuru zaidi wateja wetu kuendelea kutumia intaneti wakiwa popote pale bila kuwa na hofu ya hata kama ameishiwa bando. Wateja wa Airtel kote Tanzania watatakiwa kupiga *149*99# ili kufurahi bei hizi mpya na kufuata maelezo ya fuatayo,

· Changua namba 5

· Kisha changua namba 11 na kuanza kuperuzi.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema, ‘Airtel iko tayari kutoa huduma ambazo zinapatikana kwa urahisi na nafuu kwa wateja wake na kwa sasa kuperuzi kwenye mtandao imekuwa ni rahisi sana, wateja wetu kwa sasa wanaweza kubakia kwenye mtandao hata kama bando lake limeisha. Tunaamini ya kwamba kwa bei zetu hizi mpya wateja wetu wataendelea kuwasiliana na marafiki pamoja na wanafamilia kwa uhuru zaidi huku wakiokoa fedha zao na kuzitumia kwa maendeleo yao zaidi.’

“Airtel inaendela kutoa huduma za intaneti ambazo ni nafuu nchini kote ambapo sasa tunajivunia kwamba huduma ya Airtel 4G inapatikana kwenye mikoa 24 nchini pamoja na miji mikubwa yote. Nia yetu ni wateja wetu waendelee kutumia huduma zetu, tunawakaribisha wateja wapya kufika kwenye maduka yetu ya huduma kwa mteja au Airtel Money Branch zilizopo kila kona nchnini ili kujipatia laini ya Airtel 4G na kuanza kunufaika na huduma zetu ambazo ni rahisi na nafuu” alisema Singano.

“Kulingana na takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zalizochapishwa mwezi Machi 2020, zinaonyesha kuwa watumiaji wa intaneti hapa nchini kati ya mwaka 2014 hadi 2019 wameongezeka kutoka milioni 14.2 mpaka 25.7. kwa hali hiyo ya uhitaji inatupa msukumo sisi Airtel kama watoa huduma kuendelea kuboresha zaidi wingo wetu wa huduma za Airtel 4G pamoja na kubuni bidhaa za kisasa na kuzindua huduma mpya ili kuendana na uhitaji wa kila siku kwa wateja wetu. Singano alimalizia kwa kusema hayo
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: