Dr. Rose Leonard Shayo, mke wa Prof. Leonard Shayo mwasisi wa vijiji vya Sayansi na Teknolojia duniani ajitosa kugombea ubunge jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM. Prof. Shayo aligombea uraisi mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia Makini na alifariki mwaka 2008 mjini Arusha. Dr. Rose Shayo ni mtaalam wa Taaluma za Jinsia na Maendeleo. Dr. Rose Shayo amefundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam takribani miaka arobaini masomo ya Taaluma za Jinsia, Maendeleo na Uchumi. Wanafunzi wamejitokeza kumpongeza Mwalim wao kwa kuitikia ombi lao la kuwania nafasi hiyo. Tunamtakia kila la kheri katika safari yake ya kisiasa. Dr. Rose ana PhD ya Gender Analysis and Development Economics kutoka Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: