Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) akisaini kitabu cha wageni.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) akitoa maelekezo machache kwa watendaji.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (mwenye suti nyeusi) akipata maelezo toka kwa Kaimu Meneja wa Mawasiliano TFS, Martha Chassama (kwanza kushoto) Mara baada ya kutembelea banda la TFS.

Na Mwandishi Wetu.

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki ameupongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa jinsi ulivyojiopanga kuonesha shughuli zake ikiendana na utoaji wa elimu ya uhifadhi wa misitu, uendelezaji utalii ikologia na wa Malikale.

Pongezi hizo zimetolewa na Dkt. Nzuki mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kuijonea shughuli mbalimbali zinazoendelea katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yaliyoanza tarehe 01 - 13 Julai, 2020 katika viwanja vya Mwl. Nyerere.

Amesema ameridhishwa na namna TFS ilivyojipanga na jinsi walivyo mahiri katika kutoa maelezo kwa wananchi kuhusu shuguli zinazofanywa na taasisi hiyo na kuitaka menejimenti ya TFS kufanyia kazi mapendekezo yote aliyowahi kuyatoa kwa lengo la kuboresha utendaji wa taasisi hiyo.

“Nimefurahishwa kuona shuguli zote mnazofanya ziko bandani hapa, nimepata historia nzuri ya michoro ya Kondoa Irangi, Hifadhi za Mazingira Amani ziko hapa zikiwakilishwa na hifadhi mama Amani, lakini pia Kurugenzi ya uzalishaji mbegu za miti imeimarika na wanatoa mbegu na miche bora ya matunda na miti kwa wananchi, 

“Hakika mmejipanga hata nimeweza kuona jinsi mlivyojipanga kupambana na moto kupitia satalaiti ya kufuatilia Majanga ya moto, sasa nitowe wito kwa jamii kuungana na serikali kulinda na kuhifadhi misitu, Serikali inatimiza wajibu wake na jamii ishiriki kuhifadhi maliasili zilizopo nchini kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho,” alisema Dkt. Nzuki.

Naye, Kaimu Meneja wa Mawasiliano TFS, Martha Chassama amemshukuru naibu katibu mkuu kwa kutenga muda wake kutembelea na kutumia muda mwingi kwenye kila eneo la TFS lililopo ndani ya Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii licha ya kuwa na majukumu mengine.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: