Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 
KATIKA kukuza sekta ya michezo, kampuni ya Parimatch imezindua rasmi kampeni ya "Amsha Ndoto na Parimatch" ambayo kila mwezi kutakuwa na droo Maalum itakayowezesha timu shiriki kujipatia vifaa vya michezo kutoka kwao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Parimatch Tanzania Tumaini Maligana amesema lengo la kuanzisha kampeni hii ni kukuza, kuhamasisha na kutimiza ndoto za vijana katika sekta ya michezo hususani mpira wa miguu. 

Amesema, utaratibu utakaotumika ni kwa timu hizo kutembelea tovuti yao na kujaza fomu ya ushiriki na viambatanishw atakavyoelekezwa na kila mwezi timu 5 zitapata vifaa mbalimbali ikiwemo jezi, viatu, mipira na bibs.

"Ili timu hizi ziweze kupata nafasi zitatakiwa kutembelea tovuti yetu ya https://pma.bet/amshandoto kujaza fomu ya ushiriki na viambatanisho husika na kila mwezi tutachagua timu hadi 5 za zitakazopatiwa vifaa ikiwemo jezi, viatu, mipira na bibs."amesema Maligana 

Aidha, ameeleza kuwa kama kila mwezi zitatoka timu tano hivyo kwa mwaka watafikia karibu timu 60 jambo ambalo sio dogo katika kukuza sekta hii ya michezo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Parimatch Tanzania Tumaini Maligana akizungumzia uzinduzi rasmi wa kampeni ya "Amsha Ndoto na Parimatch" ambayo kila mwezi timu tano zitafanikiwa kupata vifaa vya michezo kutoka kwao. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: