Na Kaiza Kudura Dsj

TUME ya taifa ya uchaguzi (NEC) imekataa rufaa 25 za kupinga walioteuliwa, rufaa 15 za ambao hawakuteuliwa na kukubaliana na rufaa 15 na kuwarejesha katika orodha ya wagombe katika uchaguzi utakao fanyika Ktoba 28,2020. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, Mkurugenzi wa tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt.Wilson Mahera amesema kuwa tume hiyo inaendelea na zoezi la kupitia, kuchambua na kuzifanyia maamuzi za wagombea ubunge zilizowasilishwa na wagombea wa vyama vya upinzani, kupitia kwa wasimamizi mbalimbali wa uchaguzi nchi nzima.

Aidha amesema kuwa kufuatia kifungu cha 40(6) cha sheria ya taifa ya uchaguzi, sura ya 343 kinatoa fursa kwa wagombea ubunge kukata rufaa wanapokuwa hajaridhika na uamuzi wa wasimamizi wa uchaguzi kutokana na pingamizi zilizowasilishwa.

"Zoezi la kuzijadili na kuzitolea uamuzi rufaa hizo linaendelea na kuanzia leo, tume itakuwa inatoa uamuzi na kuwajulisha wa husika kwa kadri rufaa hizo zitavyokua zinamalizika kushughulikiwa." Amesema Dkt. Mahera

Tume ya taifa ya uchaguzi imewarejesha baadhi ya warufani kwenye orodha ya wagombea na itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kuanzia leokesho na kuendelea.

Hata hivu tume hiyo inaendele kuchambua vielelezo, nyaraka na maelezo ya warufani na warufani zilizo wasilishwa ili kuhakikisha haki inatendeka kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Kwa upande wa wahusika wa rufaa hizo NEC imeanza kuwajulisha kwa barua na maamuzi yaliyotolewa na baada ya kupitia na kuchambua nyaraka za rufaa zao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: