Rais wa TFF, Wallace Karia (katikati) na mkandarasi Yixiaobo wa kampuni ya Groupsix International wakionesha mkataba wa ujenzi wa vituo vya mpira wa miguu vya Dar ea Salaam na Tanga, mkataba uliosainiwa leo Jijini Dar es Salaam, kulia ni makamu wa kwanza wa Rais wa TFF Athuman Nyamlani.

Na Agness Francis, Michuzi TV

KATIKA kuendeleza soka la Tanzania na kufikia hadhi ya kimataifa, Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania( TFF) limesaini mkataba na kampuni ya six international Ltd ili kujenga vituo bora vya mpira hapa nchini.

Zoezi hilo la kusaini makubaliano hayo ya ujenzi wa vituo hivyo limefanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ofisi za TFF.

Makubaliano hayo yamelenga mradi huo utakaotekelezwa katika Jiji la Dar es Salaam katika maeneo ya Kigamboni, Kigamboni technical center, pamoja na Mkoani Tanga, Tanga technical center.

Mradi huo utajengwa kwa kutumia fedha za FIFA na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 12, mara baada ya kuanza kwa ujenzi huo.

Aidha Rais wa TFF Wallace Karia amesema kuwa miradi hiyo inakwenda kwa awamu na matarajio yake ni kuhakikisha kila mkoa unakuwa na vituo hivyo vya mpira.

"Mradi unakwenda kwa awamu, na katika mipango yetu tutahakikisha kila Mkoa unakuwa na kitu kama hicho,Tutatumia fedha za wadau wetu mbalimbali pamoja na wale watakaojitokeza pia." Amesema Wallace Karia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: