Mapema Asubuhi ya leo November 24, 2020 Mh. Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Hamisi Shabani Taletale @babutale alitembelea katika kituo cha Afya Mkuyuni kuwaona wagonjwa na amekuta wakiendelea vizuri na matibabu na Kinamama wamejifungua salama.
Pia Mh. Mbunge ameweza kutoa msaada wa Bima ya Afya ya NHIF kwa watoto 50 na Wazee 50 ambao walikuwa hawana bima za Afya.

Uongozi wa Kituo cha Afya Mkuyuni, wameshukuru kwa Mbunge kuwatembelea na kusema kuwa wanaendelea vizuri lakini pia wangependa kupata mashine ya X-ray pamoja na sehemu ya Kupumzikia.

Mh. Mbunge amewambia kuwa eneo la kumpumzikia ni ahadi yake kutoka katika mfuko wa Jimbo na kuhusu mashine ya X-ray amesema kuwa atapambana kulisogeza juu kwenye uongozi. 

#MorogoroMpya #TaleWawote
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: