Mkurugenzi wa REPPSI Edwick Mapalala akiwa katika maonyesho ya siku ya ukimwi katika viwanja vya Posta, Kijitonyama
Mkurugenzi wa REPPSI Edwick Mapalala akiwa na baadhi ya vijana katoka maonyesho ya siku ya ukimwi katika viwanja vya Posta, Kijitonyama
Mwandishi wetu, Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika Regional Psychosocial Support Initiative (REPPSI), Edwick Mapalala ameikumbusha jamii kuongeza upendo na kuendelea kutokomeza unyanyapaa kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).

Amesema kuwalinda, kuwathamini na kuwajali watu wanaoishi na VVU hasa vijana kutasaidia kuwapunguzia msongo wa mawazo wale ambao hawajaikubali afya yao, na hivyo kuikubali na kushiriki katika kukuza uchumi wa Taifa.

Mapalala amesema hayo wakati akitoa salamu za REPPSI, Shirika linalojihusisha na malelezi, makuzi na msaada wa Kisaikolojia kwa watoto kuhusu siku ya Ukimwi Duniani.

“Hii ni siku ya kutafakari kuhusu maambukizi ya VVU, waliopima na kujua afya zao waendelee kuwa waaminifu kwenye utumiaji wa dawa, wasiopima wapime ili wajitambue na wale wasio na maambukizi waendelee kujilinda. Pia tuwakumbuke waliopoteza maisha yao kwa VVU,” amesema Mapalala.

Akizungumzia mradi wa Ready Plus, unaowahusu vijana wanaoishi na VVU Mapalala amesema wengi wamejikubali, wanajiamini na wanaendeleza ndoto zao za kimaisha baada ya kupatiwa elimu sahihi kuhusu VVU
.
“Na nitoe wito kwa jamii, tuendelee kuwalea vijana wetu kwa upendo, tusiwakatishe tamaa kwa sababu wanaweza kufikia ndoto,” amesema Mapalala.

Hata hivyo ameipongeza Serikali ya Tanzania kwajitihada kubwa katika kupambana na VVU.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: