Msafara wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ukipita katika barabara ya Airport kuelekea katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwa ajili ya shughuli za kuagwa na maelfu ya Wananchi wa mkoa wa Mwanza na mikoa jirani leo tarehe 24 Machi 2021.


Msafara wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ukiwasili katika uwanja wa CCM Kirumba kwa ajili ya shughuli za kuagwa na maelfu ya Wananchi wa mkoa wa Mwanza na mikoa jirani leo tarehe 24 Machi 2021.


Makamanda wa JWTZ wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 24, 2021.


Mwili wa hayati Dkt. John Pombe Magufuli, ukiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, Machi 24, 2021. PICHA NA IKULU
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: