Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida Dkt. Denis Nyiraha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi.

Na Dotto Mwaibale, Singida

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida umempongeza Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kwa kuteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida Dkt. Denis Nyiraha alisema uteuzi huo wa Bashiru ni sahihi kutokana na kazi nzuri alizozifanya ndani ya chama kwa nafasi ya Katibu Mkuu.

Nyiraha alisema Bashiru akiwa Katibu Mkuu wa CCM alifanikiwa kurejesha mali za chama zilizokuwa mikononi mwa watu wengine kinyume na utaratibu.

" Pamoja na kuzirejesha mali hizo Bashiru alifanikisha chama hicho kupata ushindi katika uchaguzi wa Serikali za mtaa uliofanyika mwaka juzi ." alisema Nyiraha.

Aidha Nyiraha alisema katika kukiongoza chama hicho kwa nafasi hiyo ya Katibu Mkuu CCM ilipata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi mkuu 2020.

Nyiraha alitaja mafanikio mengine ya Dkt.Bashiru kuwa ni kusimamia nidhamu ya utumishi ndani ya chama na nje ya chama.

" Hakika tunayo imani Dkt. Bashiru ataisimamia Serikali ipasavyo kutimiza majukumu yake kama alivyofanya akiwa katika nafasi hiyo kubwa ndani ya chama." alisema Nyiraha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: