Kuna baadhi ya wanaume hawajui jinsi ya kuzungumza na mwanamke au msichana. Kwa njia hii wanaume wengi wanaishi maisha ya bila kumvutia mwanamke yeyote. Hapa kuna njia 10 utakazozitumia wewe mwanaume ili kuhakikisha humkwazi mwanamke unayempenda mnapokuwa katika mazungumzo nae...

1. Wakati ukizungumza nae, jaribu kuzungumzia "hisia" kama vile kumbu kumbu yako ya utotoni, matarajio ya baadae au matamanio yake. Mada hii ya mazungumzo yenu yatafungua milango ya hisia zake ghafla.

2. Wanawake huhitaji mwanaume asiyekuwa na uoga wa kuwamiriki na kuwaongoza. Wakati unazungumza na mwanamke tawala mazungumzo yenu, kamwe usimpe nafasi ya yeye kuanza kufikiri, kuwa nini uchokuwa ukizungumza.

3. Kuwa makini wakati unapokuwa ukizungumza naye kwa majibu yasiyo na anayokuwa akikujibu, na kama kwa bahati mbaya ukonaye karibu kiasi cha kugusana, basi jisogeze pembeni wakati ukiwa unaendelea kuongea ili asishtukie au unaweza kumuona hayuko sawa katika utoaji majibu... kwa kawaida atakuonyesha ishara, hivyo kuwa nazo makini.

4. Kumbuka hii kauli mbiu "Ucheshi/vituko si mapenzi". Wanawake huvutiwa sana na wanaume wanaoweza kuwafanya wawe na furaha muda wote. Usijikite zaidi katika kufanya utani unaopita kiasi na kusahau ulichokuwa unaongea. Bali jikite zaidi katika mambo yanayomfanya ajisikie kuwa na msisimko na starehe wakati ukonae.

5. Zama katika undani wa mazungumzo baina yako na yeye. Mwanamke huendana na mwanaume asiyekuwa muoga wa kuzungumzia mambo binafsi kwa ukaribu.

6. Wanawake wengi hupenda kujua maoni yako kuhusiana na jinsi unavyomuona. Mwambie vitu unavyoviona kutoka kwake, lakini jaribu kuwa makini ili usitamke vitu vingine vitakavyo msababishia apoteze furaha.

7. Epuka kumpa ofa nyingi mwanamke, mwanamke huwa na mashaka na mwanaume anayempatia vitu vingi kwa wakati mmoja ama kila mara. Kwasababu atafikiri vitu unavyompatia ni kutaka kumvutia tu ili umpate kiurahisi. Kitu ambacho baadae kitaleta madhara makubwa.

8. Kama unahitaji kujua njia nzuri ya kuweza kuongea na mwanamke au msichana bila kumfanya asichikie au kuboreka, basi usitumie njia ya kumuuliza maswali mengi katika mzungumzo yenu. Bali cha zaidi jaribu kueleza mawazo yako kuhusu vitu flani.

9. Kumbuka kauli juu ya kuuliza maswali: Badala ya kumuuliza "wewe umekulia wapi?", uliza "unaonekana kama hujakulia maeneo haya!" Hii itakusaidia wewe kufanya uchunguzi juu yake bila yeye kujua.

10. Usifiche utambulisho wako - zungumza vitu kutoka katika hisia zako, onyesha uhalisia wako katika kuzungumza na usitumie mikogo ya mtu yeyote.

Njia bora ya kufikiria jinsi ya kuzungumza na mwanamke, ni kutambua njia sahihi ya mazungumzo ya furaha na yakimahaba utakayopenda kuitumia, usimuige mtu. Kuzungumza na mwanamke si vigumu bali nikujua ni vitu gani hasa mwanamke hapendi kuvizungumzia na vitu gani anapenda kuvisikia. Fuata maelekezo hapo juu utaona matunda yake... kisha rudi utoe maoni yako.

MUHIMU: Maelekezo haya yote yatafanikiwa kwa mwanamke mwenye kuhitaji mapenzi ya kweli - yani sio kwa wanawake wanaolenga kuchota pesa kwako na kutokomea. Hivyo kuwa makini sana
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

13 comments:

 1. The article was very helpful to me, I thank you for creating this article.

  ReplyDelete
 2. Holy f#ck it helped me men

  ReplyDelete
 3. Msaada jamani kuna mdada nampenda lakini yupo makiní na anaishí maisha yake kama mwanaume nifanyeje nimpate

  ReplyDelete
 4. Gud men it helpfull.

  ReplyDelete
 5. Tanx bob really it worked on me

  ReplyDelete
 6. HABARI HII NI NZURI SANA MAANA INALETA MAWAZO MAPYA JUU YA KUONGEA NA MWANAMKE KWA KUWA HUWA WANAJISIKIA SANA PALE UNAPOANZA KUONGEA NAE KANA KWAMBA HAWATAKI KUMBE WANATAKA. JE MWENYE PESA INAKUWAJE KAKA

  ReplyDelete
 7. Godlisten Masanja19 June 2016 at 22:00

  KUNA WANAWAKE HAWAJUI KURUDISHA, KWA MFANO UNAWEZA UKASEMA NAOMBA MAJI SISTER AKASEMA WE HUYAONI JE NIFANYEJE KATIKA HILO WAKATI SASA NAMPENDA

  ReplyDelete
 8. Siku hizi nilipe nisepe.afu wakati mwingine Hawa wasichana ni wehu anawezampenda muhuni hana hata mia akipata kuvuta bangi lakini bado atang'ang'ana apoapo..

  ReplyDelete
 9. habari nzuri lakini sisi wanaume atujuwe ginsi yaku sogelea mwanamke na kuongea ,

  ReplyDelete
 10. jamani kuna mwanamke nampenda ila ananiambia ana mpenz wake yaani mm kwake nimekufa ebu mnishauri nifanyaje

  ReplyDelete