Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Mara Group Bw. John Staley akiongea na wateja, wadau na wafanyakazi wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam hivi karibuni, kwa lengo la kusisitiza ahadi ya kuendelea kutoa bidhaa za kipekee haswa kwa “retail banking” ambayo anajivunia uzoefu wake. Stejini ni muwakilishi wa wanahisa Bw. Michael Wilkerson, Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa BancABC Bw. Imani John.
Muwakilishi wa wadau wa BancABC Bw. Michael Wilkerson, akizungumza na wateja pamoja na wadau wa BancABC wakati wa mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena Dar es Salaam. Mkutano huo ulikuwa mahususi kwa ajili ya kusisitiza juu ya ahadi ya BancABC kuendelea kutoa na kutengeneza bidhaa bora kwa ajili ya wateja wake.
Katika picha ya pamoja, toka kulia Mkurugenzi mtendaji wa Atlas Mara Group Bw. John Staley, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Bw. Imani John pamoja na muwakilishi wa wanahisa wa BancABC Bw. Michael Wilkerson.
Wafanyakazi wa BancABC katika picha ya pamoja baada ya hafla yenye mafanikio iliyoandaliwa na BancABC
Wateja wa BancABC walipowasili kwa ajili ya hafla. Hafla hii iliwaleta pamoja wadau, wateja, uongozi pamoja na wafanyakazi wa benki.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: