Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa ya kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kipindi chote cha kampeni za uchaguzi Jimbo la Ukonga hadi uchaguzi uliofanyika siku ya Jana na kumalizika salama pasipo uvunjifu wa amani.

RC Makonda ametoa pongezi hizo leo alipokutana na Makamanda na maafisa wa polisi ambapo amesema anajivunia kuona uchaguzi wa Ukonga umemalizika salama bila fujo wala uvunjifu wa amani.
Aidha RC Makonda amewapongeza wananchi kwa kulinda aman na kulifanya jiji la Dar es salaam kuzidi kuwa na amani masaa 24.

Pamoja na hayo RC Makonda amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na Kamanda wa PolisI Kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa kwa kuwa na vijana shupavu, wakakamavu na wenye morali ya kuwatumikia wananchi.
Askari wa Jeshi la Polisi wakimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: