MCHEZAJI wa Klabu ya Simba Middie Kagere amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Agosti wa Ligi kuu Tanzania bara (TPL) msimu huu 2018-19.

Mshambuliaji huyo anayevalia jezi namba 10 katika kikosi hicho ambacho maskani yake iko mtaa wa Msimbazi Kariakoo jijini Dar es Salaam ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashida wenzake wawili.

Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF)limesema kuwa wachezaji hao waliokuwa wakiwania nafasi hiyo ni Joseph Mahundi ambaye ni mchezaji wa Azam FC pamoja na Omary Mponda wa Kagera Sugar alioingia nao fainali katika kinyanyang'anyiro hicho.

Hata hivyo raia huyo wa kigeni kutoka Rwanda alikuwa akiongoza kwa kufunga magoli msimu huu ambapo katika mtanange wa kwanza dhidi ya Tanzania Prison alifunga goli moja,

Ambapo pia alipata mabao mengine mawili walipocheza na vijana wa Mbeya city hapa Jijini Dar es Salaam katika dimba la Taifa,

Hata hivyo rekodi yake imevunjwa na mchezaji wa Stand United Hakizimana Kitenge ambaye ni raia wa Burundi aliefunga hat-trick rekodi ya kwanza msimu huu jana dhidi ya Yanga.

Kagere ambaye ndio mara ya kwanza anachezea Ligi Kuu ya Tanzania (TPL) akitokea katika kikosi cha Gor Mahia nchini Kenya alikokuwa akikipiga kabubumbu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: