Na Ripota Wetu, Globu ya Jamii.


NI pigo!Ndivyo unavyoweza kuelezea taarifa za kufariki dunia kwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM),Dkt.Misanya Dismas Bingi.


Dkt. Misanya ambaye pia amewahi kuwa mtangazaji maarufu nchini wa Radio One na ITV amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbii Aminiel Aligaeshi amesema Dkt. Misanya amefia MOI ila mwili wake umehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti Muhimbili.

Dkt.Misanya Bingi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.Alifikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kupata ugonjwa wa kupooza(stroke) na kupelekwa katika chumba cha Uangalizi maalum (ICU).

Kwa sasa msiba upo eneo la Makongo Juu jijini Dar es Salaam wakati taratibu nyingine zikiendelea.

Tunatoa pole kwa Watanzania wote, familia, ndugu, jamaa na marafiki kutokana na msiba huo mzito wa kuondokewa na mpendwa wao Dkt. Misanya Bingi.

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa jina lake libarikiwe., AMEN.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: