Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi mchana Septemba 20, 2018 imefikia 151 huku uokoaji ukiendelea.

Akiwa kwenye eneo la tukio, Mtangazaji wa TBC1 Enock Bwigane amesema ameona miili 15 ikiwa inaopolewa.

Jana, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe alisema idadi ya waliokufa kwenye ajali hiyo ilikuwa watu 136 hivyo pamoja na iliyoopolewa leo inafanya idadi ya walioopolewa kufikia 151.

Akizungumza akiwa katika eneo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema miili mingine imeopolewa leo asubuhi Septemba 22, 2018.

“Leo miili mingine imeopolewa lakini bado uopoaji unaendelea,” amesema.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: