"Asenga anaandika mimi nilikuwepo ndani ya kivuko kile cha Mv. Nyerere, tumepona tu kwa sababu tulikuwa nje,waliokaa ndani ni ngumu sana kupona kwakuwa kivuko kiligeuka gafla chini juu na kina uzito, mtu ukifunikwa vile ata waokozi wakifika ndani ya robo saa kukuta bado mzima ni ngumu sana.

Kama hauamini na unazani masihara jaribu kuzama ndani ya pipa la maji kwa dakika 10 bila kupumua uone.

Mimi naomba wale waliozidisha abiria na uzito wakamatwe kama Mhe Rais alivyosema na sisi abiria tujiongeze

Tukifika standi kwenye basi ama bandarini tuwe tunauliza, je hiki kivuko kina beba watu wangapi?

na huo uzito ubandikwe kwenye mbao za matangazo,ukiona watu wamezidi usipande ila wa afrika sisi tunalazimisha na wengine tunatoa rushwa ili turuhusiwe kupanda madhara ndio haya,

ni ngumu sana kupona ukifunikwa vile ata kama baada ya dakika 10 kivuko kinge ondolewa majini lazima maiti zingekuwa nyingi sana,

watu waangalie ata Marekani boat ili wahi kuzama kwa kugeuka tu watu 17 wakaaga dunia,,waokozi wanafika wakakuta tayari na wenzetu wameendelea sana lakini kifo cha maji kinaua haraka hasa kama mtu unakuwa umefunikwa kama hawa walikuwa ndani.

Hiki kivuko kime karabatiwa mwaka jana na kote huko kimeenda vizuri tu tunakaribia kupaki watu wa ndani wanagombea kutoka nje kwa kuwa watu walizidishwa uzito ukaenda sehemu moja kikageuka wajuu tukarushwa kwenye maji ndio pona yetu, wavuvi jirani wakaja kutuokoa, walipoingia ndani ya kivuko kwa chini mda ule ule wakakuta watu washakufa kwa kukosa hewa sasa watu wasilaumu tu bila kujua.

nawaambia usiombe kufunikwa na kivuko, Sikia tu kwenye mitandao... fikisha salam mimi John Kisekwa..."

MWENYEZI AWAPUMZISHE KWA AMANI MAREHEMU WETU

INNALILLAHIR...
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: