. Afisa uvuvi Msaidizi katika soko la samaki Feri Ahmed Mbarouk akizungumza na blogu ya jamii kuhusiana na hali ya uvuvi na biashara ya samaki sokoni hapo.
 Samaki wakiwa tayari kwa mauzo ambapo samaki mmoja huuzwa kati ya shilingi 45,000 hadi 50,000.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
 Mnada wa samaki ukiendelea katika soko la samaki la Feri jijini Dar es Salaam.
Mwandishi kutoka Blogu ya jamii akiangalia samaki aina ya kaa mara baada ya kuvuliwa na mmoja wa wavuvi. (Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii).

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

UVUVI na uuzaji wa samaki katika soko la Feri jijini Dar es salaam umezidi kuimarika katika mchakato mzima wa uvuvi wa samaki wenye viwango vinavyotakiwa na uuzwaji wake sokoni umekuwa na tija.

Akizungumza na blogu ya jamii Kaimu Afisa Uvuvi wa soko la Feri Ahmed Mbarouk ameeleza kuwa upatikanaji wa samaki kwa sasa ni mzuri hasa kwa samaki wakubwa na hata mauzo yamekuwa mazuri pia kutokana na ubora wa samaki wanaovuliwa kuwa na viwango.

Kuhusiana na kutokomeza uvuvi haramu Abdallah ameeleza kuwa kwa sasa hakuna matukio hayo ya wavuvi kutumia baruti kuvua samaki na hii ni baada ya kampeni waliyoiendesha na kufanikisha kukamatwa kwa nyavu haramu kubwa 14 aina ya kokoro ambazo ziliteketezwa.

Akieleza changamoto wanazokabiliana nazo kiutendaji Afisa uvuvi huyo amesema kuwa vifaa vya kazi hasa boti la doria limekosekana hali inayowapelekea kufanya doria kwa miguu licha ya kuwa na askari wa Suma JKT wanaosaidia na kueleza kuwa boti hilo likipatikana litawarahisishia kazi ya kufanya doria nyakati zote na kwa uhuru zaidi.

Aidha ametoa wito kwa kwa wavuvi kwa kuvua samaki wenye viwango vinavyofaa na doria hizo ni endelevu hivyo wavuvi wafuate kanuni na taratibu.

Mmoja wa wavuvi hao Jumanne Ramadhani amesema kuwa wanaushukuru uongozi wa soko hilo hasa maafisa uvuvi kwa kuwapa elimu na kuwasimamia kwani hadi sasa wanajua viwango vya samaki wanaotakiwa kuvuliwa na kupelekwa sokoni na kwa sasa biashara ni nzuri kwani upatikaji wa samaki hasa wakubwa umekuwa mkubwa na soko kwa ujumla limesimama imara.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: