Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kuutaarifu Umma kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atakuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za ufunguzi wa Flyover ya Mfugale katika makutano ya barabara za Mandela na Nyerere eneo la TAZARA tarehe 27 Septemba, 2018 jijini Dar es Salaam.

Ujenzi wa Flyover ya Mfugale ulianza tarehe 15 Oktoba, 2015 ambapo jiwe la msingi liliwekwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli tarehe 16 Aprili, 2016.

Flyover ya Mfugale inajumuisha barabara mbili za juu; moja kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kuelekea katikati ya jiji na nyingine kutoka katikati ya jiji kuelekea Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Kukamilika kwa Flyover ya Mfugale kutapunguza msongamano wa magari katika eneo la TAZARA na kupunguza muda wa safari toka katikati ya jiji kwenda Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa wa Julius Nyerere na kurudi, na pia kurahisisha usafiri na usafirishaji kwa watumiaji wa barabara za Mandela na Nyerere.

Wananchi wote mnakaribishwa katika ufunguzi huo.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
26 Septemba, 2018

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: