Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk akifungua mafunzo ya siku 3 kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutoka katika maeneo yenye uchaguzi mdogo wa Ubunge na udiwani utakaofanyika katika jimbo la Liwale na kwenye kata 37 leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya siku 3 kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutoka katika maeneo yenye uchaguzi mdogo wa Ubunge na udiwani utakaofanyika katika jimbo la Liwale na kwenye kata 37.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Emmanuel Kawishe akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisheria wakati wa mafunzo ya siku 3 kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutoka katika maeneo yenye uchaguzi mdogo utakaofanyika Oktoba 13 mwaka huu.
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk (katikati) wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa Mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi Mdogo, jijini Dodoma.
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi washiriki wa Mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi Mdogo, jijini Dodoma leo.
---
Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Oktoba 13 mwaka huu katika jimbo la Liwale na kwenye Kata 37 za Tanzania Bara wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni za uchaguzi.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku 3 kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutoka katika maeneo yenye uchaguzi.

Jaji Mbarouk amewataka Wasimamizi hao kufanya kazi kwa ufanisi, uhuru, uwazi na bila kuegemea upande wowote ili uchaguzi huo ufanyike kwa amani na utulivu.Amesema uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali zinazopaswa kufuatwa na kuzingatiwa akisisitiza kwamba hatua na taratibu hizo ndiyo msingi wa uchaguzi mzuri wenye ufanisi usio na malalamiko au vurugu.

“Tunakutana hapa ili kwa pamoja tubadilishane uzoefu, tujadili namna ya kufanikisha zoezi la uchaguzi lakini pia namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika hatua zote za uchaguzi, natumaini mtatumia fursa hii kubadilishana uzoefu katika kutekeleza jukumu hili lililo mbele yenu” Amesema Jaji Mbarouk.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: