Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Isack Nchunda (katikati), akizungumza na waandishi wa habri, Dar es Salaam kuhusu gawio la Shilingi 1.4bilioni litakalo gawiwa wateja wa kampuni hiyo. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando na Meneja wa Airtel Money, Ibrahim Malando.

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, akizungumza na waandishi wa habri, Dar es Salaam kuhusu gawio la Shilingi 1.4bilioni litakalo gawiwa wateja wa kampuni hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Airtel Tanzania, Isack Nchunda.
---
Kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania inatarajia kutoa jumla ya TZS1.4 bilioni kama gawio kwa wateja wake wanaotumia huduma ya Airtel Money.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wakutangaza hatua hiyo, Mkurugenzi wa Masoko na Airtel Money Bw. Isack Nchunda alisema kuwa gawio hili litatolewa kwa wateja wote wa Airtel Money pamoja na mawakala nchini kote ambao wamekuwa wakitumia huduma ya Airtel Money kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka ambayo ni miezi mitatu yaani (Junuari mpaka Machi mwaka huu).

Airtel Money tumekuwa tukitoa gawio katika kila robo ya mwaka tokea mwaka 2015. Kwa robo hii, jumla ya 1.4 TZS bilioni zitatolewa kwa wateja wa Airtel Money pamoja na Mawakala. Wateja wa huduma ya Airtel Money pamoja na Mawakala watakuwa na Uhuru wa kuchangua jinsi ya kutumia fedha zao, alisema Nchunda.

“Hii ni mara ya sita kwa kampuni ya Airtel kutoa gawio kwa wateja wote kupitia huduma yake ya Airtel Money. Kila mteja wa Airtel Money atapokea gawio hili tunalotoa kulingana na salio la Airtel Money ambalo anakuwa nalo kila siku katika akaunti ya Airtel Money. Mpaka sasa, kiasi cha bilioni 17 TZS Kimekwishatolewa kama gawio kwa wateja wa Airtel Money, aliongeza Nchunda.

Sambamba na Kutoa Gawio tunapenda kuwafahamisha wateja wetu wote wa Airtel Money kuwa huduma yetu sasa imeboreshwa Zaidi. Sasa tumewapa uwezo Kurudisha Miamala endapo watatuma fedha kwa makosa. Kurudisha Muamala uliotumwa kwa makosa mteja anapiga *150*60# na kisha chagua akaunti yangu na kuchagua rudisha muamala. Pia wateja wa Airtel Money wanaweza kuhifadhi Kumbu kumbu ya namba wanazotumia mara kwa mara kutuma fedha au namba za Kampuni zinanazo tumika kulipa bili mbali mbali. Huduma hizi mbili ni maboresho muhimu sana kwa wateja wetu ambayo yatasaidia kupunguza kukosea miamala na kumfanya mteja aweze kutumia Airtel Money kwa urahisi Zaidi.

Kwa upande wake, Meneja wa Airtel Money Ibrahim Malando alisema kuwa kuanzia sasa kila mteja wa Airtel Money ataweza kupata gawio lake kupitia akaunti yake ya Airtel Money na atakuwa na Uhuru wa aidha kutoa kwa matumizi yake au kutumia kwa kulipia bili mbali mbali kama kununua kifurushi, muda wa maongezi, LUKU na huduma nyingine nyingi.

Mawakala wa Airtel Money watapokea gawio kupitia akaunti zao za Airtel Money kama kawaida na hivyo nawaomba waendelee kutoa huduma bora kwa wateja wetu ili waendelee kufurahia kupata gawio katika robo nyingine ya mwaka inayokuja, aliongeza Malando.

Kulingana na Malando, Airtel Money imejidhatiti kuhahakisha kuwa inaendelea kutoa huduma bora ya kutoa huduma ya fedha kwa njia ya simu za mkononi na kuwa suluhisho kwa malipo ya biashara ya aina yeyote ile. Vile vile, kulingana na taarifa ya hivi karibuni toka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Airtel Money ndio huduma inayokuwa kwa kasi hapa nchini.

Airtel Money ni huduma inayopatikana kwa urahisi sana na ubunifu wa hali ya juu. Ni kwa kupitia Airtel Money pekee ambapo mteja anaweza kutuma, kupokea na kutoa fedha bure na vile kufaidi mikopo ya papo kwa hapo ya Airtel Money Timiza.

“Tunaendelea kuongeza mawakala kupitia usambazaji wa vioski vya Airtel Money na kuongeza Maduka ya Airtel Money Branch ambayo sasa tayari yanatoa huduma kama wakala wa kawaida na pia kama wakala mkubwa ambapo hadi sasa hivi tumeshafungua matawi (Airtel Money Branch) zaidi ya 400 yanayotoa wigo mkubwa zaidi wa mawakala nchini. Ni imani yetu tutaendelea kuwafikia wateja wengi zaidi kadri muda unavyokwenda.

Airtel Money inawezesha malipo mbalimbali yakiwemo yale ya huduma za serikali ( e-government) ambayo wateja wanaweza kufanya hayo malipo popote kwa wakati mmoja. “Pia huduma ya Airtel Money imeunganishwa na mabenki zaidi ya 40 nchini ili kurahishishia wateja kufanya miamala mbali mbali kama vile kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti ya benki na kutuma kwenye akaunti ya Airtel Money muda wowote na sehemu yeyote ile”.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: