Kaimu Mkurugenzi wa Uuguzi MOI, Fidelis Minja (Kulia) akiwakabidhi dawa na zawadi nyingine wazazi wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wanatibiwa katika Taasisi hiyo. Wengine ni viongozi kutoka kwenye kurugenzi hiyo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Baadhi ya viongozi wakiandaa dawa pamoja na zawadi nyingine kabla ya kukabidhiwa
Kaimu Mkurugenzi wa Uuguzi MOI akijadiliana na viongozi wa kurugenzi yake kabla ya kutoa msaada kwa watoto
Viongozi wa kurugenzi ya Uuguzi wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi
Viongozi wa kurugenzi ya Uuguzi wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi
Kaimu Mkurugenzi wa Uuguzi Fidelis Minja akizungumza na waandishi wa habari (Pichani hawapo)

NA KHAMISI MUSSA

Viongozi wa kurugenzi ya Uuguzi wa Taasisi ya Mifupa MOI leo wametoa msaada wa kijamii pamoja na dawa kwa watoto wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi wanaopata huduma katika Taasisi ya MOI wodi 5A. Msaada huo umetolewa ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha jamii kujitolea kwa wale wenye mahitaji maalumu pamoja na kuhamsisha huduma bora kwa wateja

Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi wa MOI Bwana Fidelis Minja amesema imekuwa ni utamaduni wa kurugenzi hiyo kufanya shughuli za kijamii kwa lengo la kuonyesha mfano kwa jamii na pia kuwaunga mkono wanajamii ambao hujitolea kwa ajili ya watu wenye uhitaji hususani wagonjwa

“Sisi kama viongozi wa Kurugenzi hii ya Uuguzi tumeamua tutoe msaada kwa Watoto hawa wenye vichwa vikubwa pamoja na kuwapatia dawa ambazo tumenunua kwa kuchangishana fedha zetu, pamoja na msaada huu tutawahudumia na kuwapa faraja wazazi wao. Tunaamini hili ni jambo jema kama ambavyo wengine wamekuwa wakifanya” Alisema bwana Minja

Bwana Minja ameongeza kwamba hii ni sehemu ya utakelezaji wa mpango mkakati wa Taasisi ya MOI ambao pamoja na mambo mengine unaelekeza juu ya uboreshwaji wa huduma za uuguzi pamoja na kutoa huduma bora kwa wateja yaani ‘Customer care’

“Tumefanya hivi ikiwa ni sehemu ya kuonyesha kwa vitendo kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali yetu pamoja na kazi kubwa inayofanywa na kiongozi wetu wa MOI Dkt Respicious Boniface ambaye amejitoa kwa dhati kuboresha hali ya utoaji huduma kwa wateja” Alsiema Bwana Minja

Kwaupande wake muwakilishi wa wazazi wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi Bi Zuena Ally amesema anaishukuru Serikali kwa kuboresha huduma na pia anawashukuru wauguzi ambao watoa msaada pamoja na dawa kwaajili ya Watoto

“Nawashukuru sana kwa kuteletea dawa, tulizoea kuona watu kutoka nje ndio wanatuletea msaada lakini leo mmekuja nyie, Mungu awabariki sana kwa moyo wa upendo.Mtoto wangu anaendelea vizuri nashukuru sana kwa huduma nzuri” Alisema Bi Zuena.

Taasisi ya MOI ipo kwenye utekelezaji wa mpango mkakati wake wa miaka 5 ambao pamoja na mambo mengine umejikita katika kuboresha huduma kwa wagonjwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: