Askofu Mkuu wa Kanisa la Jeshi la Wokovu Colonel Wayne Bungay akizungumza na wahitimu waliomaliza mafunzo ya Hotelia kwenye Chuo cha VETA yakiwa ndani ya  mradi wa Kanisa hilo, Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeka John Bwana na Kushoto ni Rais wa vyama vya wanawake wa Jeshi la Wokovu Tanzania Colonel Deborah Bungay.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana akizungumza na wahitimu na kuwapongeza kwa hatua waliyofikia ya kumaliza mafunzo ya Hotelia na kuwataka waende kujiendeleza ikiwemo na kuomba mikopo kutoka kwa Manispaa ili wajiajiri na kuacha kusubiri kuajiriwa.

Mkuu wa Chuo cha VETA Violet Fumbo amewashukuru Kanisa la Jeshi la Wokovu kwa kuona na kuthamini mchango wa vijana kwenye nchi kwa kuamua kuwapatia fursa ya kupata mafunzo ndani ya Chuo chake, jumla ya wanafunzi 49 wamemaliza mafunzo hayo na kukabidhiwa vyeti vya VETA leo Jijini Dar es Salaam.

Meneja wa mradi wa mafunzo kwa vijana, Janeth Mwang'amba alieleza mradi huo kutoka kanisa la Jesho la Wokovu na ukiwa unatarajia kuwezesha vijana 300 katika kata 5 za wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ifikapo 2021.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana akikabidhi vyeti kwa baadhi ya wahitimu wa Kozi ya Hotelia kwenye mahafali leo Jijini Dar es Salaam, jumla ya wanafunzi 49 wamehitimu mafunzo hayo.


Wahitimu wakitoa burudani.
Picha ya Pamoja na wanafunzi waliohitimu.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana amewataka maafisa maendeleo wa wilaya hiyo kuwaangalia kwa jicho la pili wanafunzi waliohitimu mafunzo VETA.

Ameyasema hayo katika mahafali ya wanafunzi 49 waliohitimu mafunzo ya Kozi ya Hotelia leo Jijini Dar es Salaam.

Bwana amesema kuwa maafisa maendeleo wanatakiwa kuwaingiza wanafunzi hao katika vikundi ili wapate mikopo na kujiendeleza kiuchumi.

Amesema kuwa, wanafunzi hawa wameweza kupata mafuno hayo kupitia Kanisa la Jeshi la Wokovu na haina budi kupata fursa za mikopo kwani ni msingi mzuri kwa maendeleo yao ya baadae.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Jeshi la Wokovu Colonel Wayne Bungay amewapongeza wanafunzi hao na kuwataka waende wakajiendeleze kupitia mafunzo hayo waliyoyapata kwani wao ni tegemeo kubwa kwa maendeleo ya taifa hili.

Colonel Bungay amesema, mradi huu umesaidiwa na watu wa Kanisa la Jeshi la wokovu Uholanzi, Kanisa la Jeshi la Wokovu Norway sambamba na Serikali ya Norway kuunga mkono na kusaidiana kwenye mradi huo.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha VETA Violet Fumbo amesema kuwa wanafunzi hawa wamepata mafunzo hayo na wameweza kufany vizuri na aanamini hawataufanyia mzaha na kuishia kuweka vyeti ndani.

Amewataka wanafunzi hao kujiajiri na kuonyesha ujuzi wao ili jamii waweze kufahamu kuwa Chuo cha VETA kinatoa mafunzo bora na yenye weledi.

Mbali na kukabidhiwa vyeti wanafunzi waliofanya vizuri waliweza kukabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke.

Wanafunzi hao ni Damian Francis katika upande wa Food Production, Najat Mgaja kwa upande wa House Keeping, Hotel Management ni Turuki Mansour, Bakery ni Edna Msabi.

Mafunzo haya yatamalizika 2021, kwa jumla ya wanafunzi 300 kutoka kata 5 za Wilaya ya Temeke kuchaguliwa katika vipindi tofauti ili kuweza kusoma katika Chuo cha Veta.

Wanafunzi hao wanatoka katika kata za Miburani, Chamazi, Toangoma, Makangarawe na Kilakala.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: