Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo katikati ni Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Moyo.
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kushoto akiingia shuleni hapo kwa ajili ya kushiriki ujenzi wa bweni la w katika shule ya msingi mbaramo yenye watoto wenye mahitaji maalum.
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akishiriki ujenzi huo.
Msingi ukiwa umechimbwa.
Sehemu ya wanafunzi wa shule hiyo wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo

WAZAZI na walezi wilayani Muheza wametakiwa kusimamia nidhamu za watoto wao ili kuepukana na suala la mmomonyoko wa maadili ambalo lina wakabili baadhi ya watoto hapa nchini. 

Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake wilayani humo ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea eneo la ujenzi wa mabweni katika shule ya msingi mbaramo yenye watoto wenye mahitaji maalum. 

Alisema iwapo wazazi watawajibika ipasavyo kuhakikisha wanasimamia maadili hayo watawasaidia vijana wao kuweza kuepukana na tabia ambazo sio nzuri ambazo wanaweza kuzipata kutokana na makundi mengine. 

Hata hivyo pia alisema serikali ya Awamu ya Tano inafanya jitihada kubwa ya kuboresha miundo mbinu ya watoto kujisomea hivyo wazazi wanapaswa kusimamia suala zima la nidham kwa wototo wao.

Kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanaasha Tumbo amesema kuwa kupitia kampeni ustawi wao ni wajibu watajenga madarasa na mabweni kwa ajili ya watoto walemavu ambayo wameshaanza kuitekeleza katika shule ya msingi mbaramo. Katika kuunga mkono jitihada hizo mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajab pamoja na mambo mengine ameahidi kutoa mifuko Saruji ili kuhakikisha mabweni hayo yanakamilika kwa wakati ili kutoa fursa kwa wanafunzi kusoma bila kuwepo kwa vikwazo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: