Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, wakijiandikisha kabla ya kuingia kwenye mkutano wao, jijini Dar es Salaam leo.
Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, wakiwa katika mkutano wao, wa Baraza Kuu la Wafanyakazi jijini Dar es Salaam leo. 
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano ya Kimataifa wa Shirika la Posta, Elia Madulesi akizungumza wakati akiwakaribisha wajumbe na wageni mbalimbali waliohudhuria ufunguzi wa mkutano wa baraza hilo.
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Hassan Mwang'ombe akitoa taarifa ya utendaji wa shirika kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwelwe (katikati), kabla waziri Kamwelwe, kuufungua mkutano wa baraza hilo, uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta, Kanali Mstaafu Dk. Haruni Kondo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Kamwelwe kuufungua mkutano wa baraza hilo. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwelwe (wa pili kushoto), akiimba wimbo wa mshikamano pamoja na baadhi ya viongozi wa shirika na viongozi wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika ufunguzi wa mkutano huo.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wakisikiliza maagizo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri Mhandisi Issack Kamwelwe (hayupo pichani), wakati akiufungua mkutano huo. Mbele kutoka kushoto ni Meneja wa Fedha, Rajabu Mng'ong'e, Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo na Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara, Mwanaisha Said.
Waziri Mhandisi Issack Kamwelwe, akizungumza na wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, katika ufunguzi huo. Kulia ni Katibu wa baraza hilo, Elizabeth Charles. 
Mjumbe wa baraza, Magreth Mabula, Mwakilishi wa Meneja wa Posta Mkoa wa Mbeya, akiuliza swali kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwelwe, mara baada ya kuufungua mkutano huo. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwelwe (katikati mbele), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa baraza hilo, mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo, ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwelwe (katikati), akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Kanali Mstaafu Dk. Haruni Kondo wakati akiondoka baada ya ufunguzi huo.
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Hassan Mwang'ombe akizungumza na wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, mara baada ya kufunguliwa mkutano huo, jijini leo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: