Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa mawasilianno Airtel Beatrice Singano akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake wa Airtel waliohudhuria hafla ya chai ya asubuhi maalum kwa kuchangisha fedha zitakazotumika kulipia BIMA ya Afya kwa zaidi ya watoto 100 ambao wazazi wao wameshindwa kulipia bima za watoto wao. Hafla hiyo ilifanyika katika makao makuu ya Airtel mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wafanyakazi wa Airtel pamoja na baadhi ya wateja wake. katika hafla hiyo zaidi ya shilingi milioni 6 zilikusanywa.
Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw Sunil Colaso akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake wa Airtel waliohudhuria hafla ya chai ya asubuhi maalum kwa kuchangisha fedhazitakazotumika kulipa BIMA ya Afya kwa zaidi ya watoto 100 ambao wazazi wao wameshindwa kulipia bima watoto wao. Hafla hiyo ilifanyika katika makao makuu ya Airtel mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wafanyakazia na baadhi ya wateja wa Airtel. katika hafla hiyo zaidi ya shilingi milioni 6 zilikusanywa.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Airtel wanaohudumia wateja maalum na makampuni wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada hafla ya chai ya asubuhi iliyoandaliwa na kitengo hicho kwa lengo la kukusanya fedha zitakazolipia BIMA ya Afya kwa zaidi ya watoto 100 ambao wazazi wao wameshindwa kumudu gharama hizo. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika makao makuu ya Airtel na kuhudhuriwa na wafanyakazia wa Airtel pamoja na baadhi ya wateja wake, zaidi ya shilingi milioni 6 zilikusanywa
Mkurugenzi kitengo cha wateja wakubwa na Makampuni wa Airtel Bw, Boniface Mwambo akiwa na  baadhi ya wafanyakazi wa wakala wa barabara nchini (Tanroad) wakati wa hafla ya chai ya asubuhi iliyoandaliwa na Airtel kitengo cha wateja wakubwa kwa lengo la kukusanya fedha zitakazotumika kulipa BIMA ya Afya kwa zaidi ya watoto 100 ambao wazazi wao wameshindwa kulipia bima watoto wao. Hafla hiyo ilifanyika katika makao makuu ya Airtel mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wafanyakazia na baadhi ya wateja wa Airtel.zaidi ya shilingi milioni 6 zilikusanywa
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia kitengo chake cha Huduma kwa wateja wakubwa wameshiriki kampeni maalum yakusaidi jamii inayojulikana kama Aitel Tunakujali kwa kuandaa hafla maalum ya Chai ya asubuhi (breakfast) iliyowakutanisha na wateja wao wakubwa kwa lengo la kukusanya fedha ili kuwasaidia watoto zaidi ya 100 ambao wazazi wao wameshindwa kumudu gharama za kuwalipia huduma za afya.

Airtel Tunakujali ni programu maalum ambapo wafanyakazi wa kampuni hiyo uchangia sehemu ya kipato chao kwa ajili ya huduma za kijamii na hasa kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Akiongea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi wa Airtel huduma kwa wateja wakubwa Boniface Mbwambo alisema kuwa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wakubwa na makampuni wameamua kuja pamoja na kukusanya fedha hizo ambazo zitaelekezwa kwenye ksaidia kufanikisha kuwapa bima afya kwa watoto 100 hapa nchini. 

‘Kama unavyoona hapa leo hawa wote ni wafanyakazi wa Airtel ambao tumeungana na baadhi ya wateja wetu ambapo tumeamua kuja pamoja na kukusanya fedha kwa lengo ya kuasaidia Jamii yetu inayotuzunguka na yenye uhitaji maalum. Kwa miaka kadhaa sisi wafanyakazi tumekuwa tukifanya hivi na kwa kweli tumeona ni kwa jinsi gani Jamii imekuwa ikiguzwa na michango yetu, alisema Mbwambo.

Tumeona ni vyema tuelekeza makusanyo yetu ya siku ya leo kwenye kusaidia afya kwa watoto ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ambayo imekuwa ikifanya kazi kwa bidii kwa kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata tiba pale atapohitaji, Mbwambo.

Mbwambo aliongeza kuwa tukio la leo la kukusanya fedha limefanikiwa sana kwani muitikio ni mkubwa mno. ‘ Natoa pongezi zangu za dhati kwa wanafanyakazi wenzangu wa muitikio na hamasa yenu mkubwa. Lazima niwaambie ya kwamba kuwepo kuweni hapai hii ya leo ndio kumeifanya tukio letu kupata mafanikio. Vile vile, napenda kutoa pongezi kwa uongozi wa Airtel, vitengo vingine na wadau wote kwa kutuunga mkono, alisema Mbwambo.

Kwa upande wake, Teddy Chamsama Meneja wa Airtel kitengo cha wateja wakubwa alisema kuwa Airtel Tunakujali imekuwa ikisaidia Jamii yenye uhitaji maalum kwa lengo la kuonyesha kujali na pia kuwafanya wajisijikie kama wenzao kwenye Jamii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: