Vyuo kuu vinafundisha elimu na havifundishi akili,wala jinsi ya kutafakari ndio maana mabinti wa vyuo vikuu wananunua zaidi vidonge vya kuzuia mimba Position -2 [P2] kuliko nyenzo za kujianda kuwa mke mwema na mama bora .

Binti wa chuo kikuu ,hazijui siku zake na kauli yao mbiu kwenye mapenzi ni "Mwagia Nje" ukimwagia ndani anameza P2.

Wanafunzi wa vyuo vikuu baadhi yao wanaongea wakiwa wamelala na Wengine lecturer anapoongea wao wamelala.

Serikali inapiga vita ya rushwa ya ngono kwenye vyuo vikuu lakini hakuna anayepinga tabia ya mabinti wa vyuo vikuu kutembea na wanaume za watu kuleta majonzi kwenye ndoa.

Nasisitiza kama wewe ni binti na upo chuo ,kama wewe umeshindwa kutunza siri je unayemuambia atapata wapi ujasiri wa kutunzia siri," raha ni kumwagia ndani sio nje.

Ukishika mimba usitoe zaa,mabingwa wa kutoa mimba ,ndoa zimejaa majonzi sababu mbegu zipo shamba liliharibiwa chuoni kwa kutoa mimba.

Elimu na maarifa ya kiroho yana thamani kubwa sana na ustawi wa vijana kuliko elimu ya chuo bila elimu ya kiroho.

Ukiona upo chuo miaka mitatu ya mahusiano yako umetembea na wanaume zaidi ya watatu ,jua chuoni umeenda kukuua mwili na kushindana mavazi sio kuwa na maarifa .

Unatembea na mume wa mtu anayevaa tai na wewe hata kufunga tai huwezi na unajiita Intellectual na unamuomba Mungu akupe kazi nzuri na mume bora.

Hongereni kwa ubora wenu wa shape nzuri ,mavazi ya thamani kubwa na simu za thamani ila kuwa na degree na kupata second upper haimanishi umeelimika. #Adabu

Beberu ©Benjamin James
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: