Kulia ni Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd wakati akifanya ziara katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akimwelezea Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd kuhusu shughuli za uzalishaji zinazofanyika mgodini.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akiuliza jambo.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akiongoza msafara wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd kutembelea mgodi wa Buzwagi.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akizungumza alipofanya ziara katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akishikana mkono na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd

Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akiwakaribisha wageni mbalimbali walioambatana na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd kutembelea mgodi wa dhahabu wa Buzwagi.
Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga,Mabala Mlolwa, katikati ni Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd ukitoka mgodini
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akipunga mkono kumuaga Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd amefanya ziara katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo iliyofanyika Februari 11,2019,Balozi Idd ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga alipongeza viongozi wazawa wanaoendesha mgodi huo kwa kuwekeza miundombinu ya huduma za elimu afya na barabara.

"Zamani nilikuwa nasikia tu Buzwagi Buzwagi nashukuru sana Mkuu wa Mkoa nashukuru sana Meneja Mkuu wa Mgodi kwa fursa hii ya kuja kutembelea katika Mgodi wenu lakini kitu kinachonifurahisha ni huduma kwa jamii ya hapa Kahama mmenionyesha skuli ‘shule’mlizokarabati,barabara,na kadhlika.

Pia nimeambiwa kuna hospitali mnajenga hayo yote kwa kweli ni kitu kizuri kwamba rasilimali hii inafaidisha vile vile wanajamii nawapongezeni sana muendelee ili Wana Kahama na sehemu nyingine za Mkoa wa Shinyanga waendelee kunufaika na rasilimali yao",aliongeza.

Akimkaribisha Mgodini hapo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack alisema "Mheshimiwa Makamu wa Rais Zanzibar leo tupo kwenye Mgodi huu wa Buzwagi ambao ni pamoja na mali zilizopo kwenye Mkoa ambao wewe ni mlezi tumesema upite kwenye mgodi huu ili kwa kuwa wewe ni Mlezi wa Mkoa wa Shinyanga ni muhimu uone na rasilimali zilizomo hivyo pamoja na ujumbe ulioambatana nao mtaangalia pamoja na mambo mengine uzalishaji wa Dhahabu".

Naye Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu alimshukuru Makamu wa Rais kwa kufanya ziara hapo Mgodini.

"Tumefarijika sana kupata ugeni huu tunashukuru sana, tukipata ugeni kama huu tunafurahi sana karibuni sana na kwa fursa kama hii ambavyo umeambatana na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi tunaona ni vyema tupate nafasi kukuonyesha jinsi mgodi umeshiriki katika maendeleo ya jamii na namna tunavyozalisha dhahabu",alisema Busunzu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: