Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa (mwenye tisheti nyeupe) akizungumza na mmoja ya wasimamizi wa Kichina ambaye ndiyo wanaokarabati reli ya kati kupitia kampuni ya CCECC wakati anapita  kuelekea katika ukaguzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge mwishoni mwa wiki hii. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa (wa kwanza kulia) akizungumza na msimamizi wa Kichina ambao ni wakarabati wa reli ya kati. Ambapo hapa Msimamizi huyo alikataa kuongea nao maana hajui kingereza. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa (mwenye tisheti nyeupe)  akipiga simu kwa bosi wake na huyo msimamizi wa kichina ili kuweza kuwaachia njia baada ya huyo mchina kukataa kwa madai ukarabati unaendelea.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa (mwenye tisheti nyeupe) akizungumza na wafanyakazi wa Kitanzania ambao wamepewa ajira na kampuni ya CCECC jinsi wanavyofanyakazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa (wa mbele) akiendelea kukagua ukarabati wa reli ya kati kupitia kampuni ya CCECC wakati anapita  kuelekea katika ukaguzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge mwishoni mwa wiki hii.
Shughuli ya ukarabati wa reli ya kati kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma.
Msimamizi wa Kichina wa kampuni ya CCECC akiendelea kusimamia kazi.

Baada ya kukaa kwa muda wa takribani saa 1:30 ndiyo ilipoamuliwa kuweka magogo ili treni ipite na waendelee na safari.

Treni ikipita huku ikiwa na usimamizi wa hali ya juu.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amechukizwa na utendaji kazi wa kampuni ya Kichina ya CCECC inayohusika na ukaratati wa reli ya kati.

Akizungumza mara baada ya kutembelea reli hiyo wakati akipita kukagua mradi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge, Mkurugenzi Masanja Kadogosa amechukizwa na jinsi wafanyakazi wa Kichina wanavyowabagua Watanzania wanaofanya nao kazi.

"Leo nimepita kama bahati mbaya na kukutana na haya, kiukweli sijafurahishwa na utendaji kazi wao haiwezekani watu waliopelekwa site hawajui Kingereza sasa wanawezaje kuwasimamia hawa waswahili ambao nao hawajui kichina???," amesema.

Ameongeza kuwa Kampuni iliyopewa tenda ya kukarabati reli ya Kati ya CCECC wamekuwa wakipeleka wasimamizi wasiojua lugha ya Kingereza jambo linalozorotesha utendaji kazi katika ukarabati huo.

Hatua hiyo ilikuja baada ya Mkurugenzi Mtendaji kupita na wasanii na kukuta wanakarabati wakati walipewa taarifa kuwa watapita na wasanii wakielekea mjini Morogoro kukagua mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge.

Katika hali iliyomchukiza Mkurugenzi Mtendaji Kadogosa ni jinsi wafanyakazi hao wa kichina walivyomdharau kwa kukataa kuongea nae eti hawamfahamu licha ya yeye kujitambulisha kwao hawakujali.

"Hivi nyie wafanyakazi kiongozi weni ni nani??? nimekuja hapa nikiwa ni Mtendaji Mkuu wa TRC lakini mnavyonijibu kama hamna kiongozi basi niwafukuze wote hata site,' amesema.

Ndipo Mtendaji Mkuu alipochukua hatua ya kupiga simu kwa viongozi wao na kuamuru waende ofisini kwake Jumatatu Februari 11, 2019 wakajieleze kwanini wanakuwa na dharau hasa kwa viongozi.

'Binafsi sijafurahidhwa na majibu ya hawa Wachina au wanatuona sisi ngozi nyeusi hatuna thamani kwao??? Niwaombe nyie viongozi wa TRC mlio pamoja na mimi... nawataka Jumatatu mje na hawa mabwana ofisini kwangu," amesema.

Hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji huyo amewaamuru wafanyakazi wote wanaokarabati reli chini ya kampuni ya kichina ya CCECC kuwa wawazi kusema kero zao ili zitatuliwe.

'Nimeambiwa kuwa wachina wamekuwa wakiwapiga na kuwatukana ila nyie mmekaa kimya hili siwezi livumilia katika shirika langu, nataka wote muwe na usawa,' Amesema.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Kichina ya CCECC wamekuwa ni wakaidi na hawajui lugha ya kingereza jambo linalozorotesha utendaji kwa vile hawaelewani na vijana wa Kitanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. Pole mkurugenzi
    Ilah nakushauri uhoji hao Chinese wanavyopata vibali vya kufanya kazi hapa nchini then utakuwa umesolve tatizo

    ReplyDelete