Tasnia ya Bongo Fleva imepata pigo baada kuondokewa na Rapa maarufu nchini, Golden Jacob Mbunda ‘Godzilla‘ ambaye amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo Jumatano, Februari 13, 2019 akiwa nyumbani kwao, maeneo ya Mbezi Salasala, Dar es Salaam.

Mwili wa marehemu umepelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam na msiba upo nyumbani kwao Salasala. 

 Taarifa za awali zimedai kuwa kabla ya kufika na umauti, Godzilla alikuwa akusumbuliwa na tumbo, presha na kisukari. 

Godzilla alizaliwa Januari 5, 1988 mkoani Morogoro na alikuwa Rapa aliyetikisa Bongo kwa ngoma zake kama Get High, King Zilla, Milele aliyomshirikisha Alikiba, First Class aliyomshirikisha Mwasiti, Stay, Masai Land na nyingine kibao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: