Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Mbunge wa Misungwi,Charles Kitwanga ambaye amelazwa katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa matibabu.Picha na IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Februari, 2019 amemjulia hali Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe. Charles Kitwanga ambaye amelazwa katika wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam kwa matibabu.

Mhe. Kitwanga alilazwa hospitalini hapo tangu tarehe 31 Januari, 2019.

Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Dkt. Juma Mfinanga amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa hali ya Mhe. Kitwanga inaendelea vizuri ikilinganishwa na wakati alipofika hospitalini hapo.

Akiwa wodini hapo Mhe. Rais Magufuli ameshiriki sala ya kumuombea Mhe. Kitwanga ilia pone haraka na amewashukuru Madaktari na Wauguzi kwa juhudi kubwa wanazozifanya kuwahudumia wagonjwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: