Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizungumza wakati alipoagiza mmiliki wa Kitalu cha Kampuni ya Uwindaji ya Green Miles Safaris Ltd, kuripoti mbele ya kamati aliyoiunda ili kueleza sakata la kuuawa Twiga katika kitalu chake na kushindwa kuvilipa vijiji 23 kiasi cha sh 329 milioni ,wananchi wameipongeza serikali kuingia kati mgogoro huo.
Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido wakiwa katika mkutano huo wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe akizungumza na kusema amekuwa akipokea vitisho kutoka sehemu mbalimbali kutokana na kuigusa kampuni hiyo lakini alisisitiza kusimamia sheria pamoja na maagizo aliyopewa na Rais John Magufuli katika kutetea wanyonge na maagizo ya Rc Gambo juu ya kutatua shida za wananchi wake hivyo atasimama kidete kuhakikisha haki inatendeka.
Mwandishi Wetu, Longido.

Wakati Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiagiza mmiliki wa Kitalu cha Kampuni ya Uwindaji ya Green Miles Safaris Ltd, kuripoti mbele ya kamati aliyoiunda ili kueleza sakata la kuuawa Twiga katika kitalu chake na kushindwa kuvilipa vijiji 23 kiasi cha sh 329 milioni ,wananchi wameipongeza serikali kuingia kati mgogoro huo.

Mkuu huyo wa mkoa akizungumza katika wilaya ya Karatu, katika hafla yakabidhi vitambulisho 10,000 kwa wafanyabiashara wadogo, alisema kampuni hiyo imekuwa ikikaidi maagizo ya serikali wilaya ya Longido kulipa madai ya vijiji jambo ambalo halikubaliki.

Gambo aliagiza viongozi wa kampuni hiyo wajitokeze mahali popote walipo ili kwenda katika tume maalum aliyounda inayoongozwa na vyombo vya ulinzi na usalama kubaini kwanini mauaji ya Twiga yameshamiri zaidi katika eneo la kitalu hicho na kwanini hajalipa kodi za vijiji kwaajili ya maendeleo zaidi ya sh, milioni 329.

"Hii kampuni wanamaneno mengi sana nawaambia hivi serikali ya awamu hii haina maneno inasimamia sheria popote walipo wajitokeze katika kamati ili kubaini mambo ambayo tumegundua awali na waache kutisha watu taarifa zao tunazo na nakwambia DC Mwaisumbe nipo nyuma yako katika hili simamia sheria na kanuni zilizopo hakuna mtu yoyote kukatisha kwa jambo lolote lazima tuchukue hatua "

Naye Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe alisema amepata matishio kutoka sehemu mbalimbali kutokana na kuigusa kampuni hiyo lakini alisisitiza kusimamia sheria pamoja na maagizo aliyopewa na Rais John Magufuli katika kutetea wanyonge na maagizo ya Rc Gambo juu ya kutatua shida za wananchi wake hivyo atasimama kidete kuhakikisha haki inatendeka. 

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido, Jumaa Mhina alisisitiza kampuni hiyo kulipa deni wanalodaiwa na vijiji hivyo sambamba na halmashauuri kulipwa malimbikizo ya madeni wanayoidai kampuni hiyo.

"Tumekwisha andika barua Wizara ya Maliasili na Utalii ili tulipwe lakini pia kuhakikisha vijiji vinalipwa" alisema

Wananchi Longido waipongeza Serikali.

Wakizungumzia maamuzi ya mkuu wa mkoa,baadhi ya wakazi wa Longido wamepongeza serikali kwa kuingilia kati mgogoro wao na mwekezaji huyo.

Julius Laizer mkazi wa Kutubeine alisema wanataka mwekezaji ambaye atatatua kero za wananchi katika wilaya hiyo na sio kuwa sehemu ya migogoro.

"Tunataka wanyamapori watusaidie kupata maendeleo hivyo tunaomba serikali kuingilia kati kudhibiti matukio ya ujangili" alisema

Peter Maleko kazi wa Mundarara alisema wanaomba serikali isaidie walipwe haki zao kutoka kwa mwekezaji kampuni ya Green Miles kwani wanadaia zaidi ya sh 11 milioni kila kijiji.

"Tunashukuru mkoa umefanyakazi lakini bado tunaomba tulipwe haki zetu" alisema.

Hivi karibuni,Mkuu huyo wa mkoa, aliunda kamati maalum kwaajili ya kuchunguza mauaji ya Twiga katika wilaya ya Longido ambapo alibaini mambo mbalimbali ikiwemo Twiga 35 kuuawa kwakipindi cha mwaka miwili katika matukio mbalimbali ikiwemo Twiga 25 kuuliwa kutokana na ujangili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: